NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Kitenzi cha umbo la TE + MO II DESU KA (Somo la 14)

Mwalimu Tufundishe

Kitenzi cha umbo la TE + MO II DESU KA (Somo la 14)

Ikiwa kitenzi cha umbo la TE na MO II DESU zinatamkwa kwa pamoja, inamaanisha ya kwamba ombi la ruhusa limekubaliwa. Kwa mfano, ikiwa unataka kumwambia mwingine, “unaweza kula,” unatumia umbo la TE la TABEMASU (kula), ambalo ni TABETE, na useme MO II DESU. Kwa hiyo unasema TABETE MO II DESU.

Ikiwa wewe binafsi ndiye unayeomba ruhusa, unaongeza
KA mwisho wa sentensi, na kusema sentensi kwa toni ya juu. Kwa mfano, ikiwa unataka kuuliza kama unaweza kula vitafunwa ambavyo viko mbele yako, unaongeza KA baada ya TABETE MO II DESU, na useme TABETE MO II DESU KA, (Je ninaweza kula?).
Ikiwa utapata ruhusa kutoka kwa mwingine, atasema DÔZO, (Tafadhali endelea). Hata ikiwa haufahamu umbo la TE la vitenzi, unaweza kuomba ruhusa ukionyesha kile unachokitaka kwa kusema II DESU KA? Watu wataelewa kile unachotaka. Ni neno rahisi kulitumia.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.