NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Vitenzi vya umbo la TA (Somo la 12)

Mwalimu Tufundishe

Vitenzi vya umbo la TA (Somo la 12)

Vitenzi vya umbo la TA ni aina ya vitenzi vilivyonyambuliwa ambavyo vinaishia na TA au DA. Ni vya wakati uliopita au wakati timilifu. Hebu nikuelezee vile unavyoweza kubadilisha vitenzi vya umbo la MASU hadi umbo la TA . Namna ya msingi ni kubadilisha MASU iwe TA. NAREMASU, (kuzoea), inageuka na kuwa NARETA. Utagundua ya kwamba NAREMASU, silabi iliyopo tu kabla ya MASU ni RE, na irabu yake ni E. Umbo hili hutumika katika vitenzi vyote vilivyo na irabu kwenye silabi inayokuja kabla tu ya MASU ambayo ni E, na baadhi ya vitenzi vilivyo na irabu kwenye silabi kabla tu ya MASU ni I.

Katika namna nyingine, sio tu unabadilisha MASU lakini pia silabi moja kabla tu ya MASU.

Ikiwa silabi kabla ya MASU ni RI, unabadilisha RI na MASU kwa pamoja, RIMASU, iwe TTA. Kwa hiyo, ATSUMARIMASU (kukusanyika), inakuwa ATSUMATTA. Kanuni hii pia inatumika, ikiwa silabi kabla ya MASU ni I au CHI. Hapa pia, unabadilisha I au CHI na MASU kwa pamoja iwe TTA.

Ikiwa silabi kabla tu ya MASU ni MI, NI, au BI, unabadilisha silabi zote na MASU na kuwa NDA. Kwa mfano, YOMIMASU (kusoma) inageuka na kuwa YONDA.

Sasa, ikiwa silabi kabla ya MASU ni KI, unabadilisha silabi KI na MASU ziwe ITA. Kwa hiyo, KIKIMASU (Kusikiliza) inageuka na kuwa KIITA. Ikiwa silabi kabla ya MASU ni GI, unabadilisha silabi GI na MASU ziwe IDA. ISOGIMASU (kufanya haraka) inageuka iwe ISOIDA.

IKIMASU (kwenda) ndiyo pekee ambayo haifuati kanuni hiyo. Inakuwa ITTA.

Kwa hakika, jinsi ya kutengeneza vitenzi vya umbo la TA ni sawa na vile unavyoweza kutengenza vitenzi vya umbo la TE, jinsi ulivyojifunza katika somo la 8 na 9. Unaweza kubadilisha TE kuwa TA, na DE kuwa DA.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.