NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Vitenzi vya umbo la kikamusi (Somo la 11)

Mwalimu Tufundishe

Vitenzi vya umbo la kikamusi (Somo la 11)

Kamusi za Kijapani zinaorodhesha vitenzi katika umbo hili. Ikiwa utatumia umbo hili, utasikika katika hali ya kawaida zaidi.

Kuna namna kadhaa ya kubadilisha vitenzi vya MASU kuwa vitenzi vya Kikamusi. Kwanza, ikiwa kitenzi kina irabu E kwenye silabi kabla tu ya MASU, unaondoa MASU, na kuongeza RU kwenye kitenzi. Kwa mfano, TABEMASU(kula) inabadilika na kuwa TABERU.

Ikiwa kitenzi kina irabu I kwenye silabi kabla tu ya MASU, kuna namna mbili ya kukinyambua.
Namna ya kwanza, unaondoa MASU na kuongeza RU. Kwa mfano, ORIMASU(kushuka) inabadilika na kuwa ORIRU.
Namna ya pili, unaondoa MASU na kubadilisha irabu I kabla ya MASU kwenye irabu U. Kwa hiyo, kwa neno IKIMASU(Kwenda), unaweza kubadilisha KI na kuwa KU, na kupata IKU.

Kuna vitenzi viwili ambavyo havinyambuliki kwa namna ya kawaida. Navyo ni KIMASU (kuja) na SHIMASU (kufanya). KIMASU inabadilika na kuwa KURU, na SHIMASU inabadilika na kuwa SURU. Vitenzi hivyo ni viwili peke yake lakini hutumika mara kwa mara . kwa hiyo tafadhali jifunze vitenzi hivyo vizuri.
Ili kujifunza namna hizo, tafadhali nenda kwenye “Nyenzo za kujifunzia.”
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.