NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > IMASU na ARIMASU (Somo la 10)

Mwalimu Tufundishe

IMASU na ARIMASU (Somo la 10)

Katika somo la 7, Anna alishangaa alipoona keki nyingi kwenye duka la kuuza keki, na akasema KÊKI GA IPPAI ARIMASU (Kuna keki nyingi). Katika muktadha huu, ikiwa kiima kinahusu vitu visivyo na uhai, unatumia ARIMASU.
Unaamua utumie ARIMASU ama IMASU kwa kuzingatia sio tu, ikiwa kitu kina uhai au la, bali pia kwa kuangalia ikiwa kinaweza kujisogeza chenyewe ama la.

Mimea ni vitu vilivyo hai, lakini haiwezi kusogea. Kwa hiyo unatumia ARIMASU kuviashiria.

Samaki wanaouzwa dukani hawawezi kusogea, kwa hiyo unatumia ARIMASU. Lakini kwa samaki anayeogelea ndani ya sanduku la maji, unatumia IMASU.

Mabasi na magari, hayawezi kujisongeza yenyewe. Lakini ikiwa yatakuwa na madereva wanayoyaendesha, tunatumia neno IMASU. Kwa kifupi, kitenzi kinachoashiria uwepo wa watu na wanyama ni IMASU. Umbo la kukanusha kwake ni IMASEN, yaani (hakuna).”

Unapozungumzia uwepo wa vitu visivyo na uhai, unatumia
ARIMASU. Ukanusho wake ni ARIMASEN (hakuna).
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.