Mwalimu Tufundishe
Mfumo wa uandishi wa Kijapani (Somo la 1)
Lugha ya Kijapani ina aina tatu ya mfumo wa herufi, kila moja ikiwa na jukumu lake. Unapoandika WATASHI WA ANNA DESU (Mimi ni Anna), nomino ya kujitambulisha yaani "mimi," WATASHI, inaandikwa kwa herufi ya Kanji.
Hiragana na Katakana ni alama za fonetiki, kila moja ikiwakilisha silabi moja. Lugha ya Kijapani ina irabu tano: a, i, u, e, o. Na ina konsonanti tisa. Kwa Kijapani kila irabu, ama konsonanti na irabu huunda silabi moja. Zaidi ya hayo, kuna "n."
Jaribu kuandika jina lako kwa Kijapani, ukizingatia mfumo wa maandishi uliopo kwenye jedwali linalopatikana kwenye kitabu cha kiada cha kipindi hiki, au kwenye tovuti hii.