Somo la 7
Kuna skonzi za krimu?
Anna na Sakura wamefika kwenye duka la kuuza keki.
Usemi wa msingi:
SHÛKURÎMU WA ARIMASU KA
Mazungumzo
アンナ | ケーキがいっぱいありますね。 | Kuna keki nyingi.
|
---|---|---|
Anna | KÊKI GA IPPAI ARIMASU NE.
Kuna keki nyingi.
|
|
さくら | すみません、シュークリームはありますか。 | Samahani, kuna skonzi za krimu?
|
Sakura | SUMIMASEN, SHÛKURÎMU WA ARIMASU KA.
Samahani, kuna skonzi za krimu?
|
|
店員 | はい、こちらです。 | Ndiyo, upande huu.
|
Muuzaji | HAI, KOCHIRA DESU.
Ndiyo, upande huu.
|
|
さくら | シュークリームを2つください。 | Skonzi mbili za krimu, tafadhali.
|
Sakura | SHÛKURÎMU O FUTATSU KUDASAI.
Skonzi mbili za krimu, tafadhali.
|
Vidokezo vya sarufi
TSU: kiambishi cha kuhesabu vitu
Ikifuatana na TSU, namna ya kuhesabu namba moja hadi kumi hubadilika.
Tafadhali nenda kwenye "Nyenzo za kujifunzia."
Mwalimu Tufundishe
Namna ya kutumia kitenzi cha ARIMASU
ARIMASU (kuna) ni kitenzi kinachoelezea kuwepo kwa vitu. Kiima cha ARIMASU kinaonyeshwa na GA.
Tanakali Sauti
Kula
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
KUDASAI ni msemo wa maana. Ikiwa nitaonyesha kitu ninachotaka kukinunua, na kusema KORE O KUDASAI (Hiki hapa tafadhali), ninaweza kukinunua, hata kama sikijui jina lake.