Somo la 47
Ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani

Muda wa masomo wa Anna wa takriban mwaka mzima nchini Japani, umekaribia kukamilika. Leo Anna atakuwa na darasa la mwisho katika chuo kikuu.
Usemi wa msingi:
NIHONGO-KYÔSHI NI NARU NO GA YUME DESU
Mazungumzo
先生 | 最後に、みなさんの夢を教えてください。 | Mwisho, tafadhali tuelezeeni ndoto zenu.
|
---|---|---|
Mwalimu | SAIGO NI, MINASAN NO YUME O OSHIETE KUDASAI.
Mwisho, tafadhali tuelezeeni ndoto zenu.
|
|
ロドリゴ | 僕は日本を1周したいです。 | Nataka kutembelea kote nchini Japani.
|
Rodrigo | BOKU WA NIHON O ISSHÛ SHITAI DESU.
Nataka kutembelea kote nchini Japani.
|
|
アンナ | 私は…日本語教師になるのが夢です。 | Kwa upande wangu... ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani.
|
Anna | WATASHI WA... NIHONGO-KYÔSHI NI NARU NO GA YUME DESU.
Kwa upande wangu... ndoto yangu ni kuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani.
|
Vidokezo vya sarufi
NI NARIMASU
(kuwa_)
NI inaonyesha matokeo ya mabadiliko.
k.m.) NIHONGO KYÔSHI NI NARIMASU.
(Nitakuwa mwalimu wa lugha ya Kijapani.)
Mwalimu Tufundishe
Namna ya kubadilisha vitenzi na kuwa nomino
Ukitaka kubadilisha vitenzi kuwa nomino, unaongeza NO au KOTO kwenye kitenzi cha muundo wa kawaida, kama vile umbo la kikamusi au umbo la TA.
Tanakali Sauti
bila matatizo
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Nimekuwa nikisoma katuni za manga za Kijapani kila siku. Sasa ninaweza kusoma SURA SURA, bila kutumia kamusi. Huu umekuwa mwaka wenye mafanikio kwangu.
