Somo la 46
Nimefurahi kuona theluji, kabla ya kurejea nchini kwangu

Baada ya kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Anna, Kenta alijitolea kumrejesha bwenini. Walipotoka, theluji ikaanza kudondoka.
Usemi wa msingi:
KIKOKU SURU MAE NI, YUKI O MIRU KOTO GA DEKITE SHIAWASE DESU
Mazungumzo
アンナ | もしかして、雪? | Hii ni theluji, au?
|
---|---|---|
Anna | MOSHIKASHITE, YUKI?
Hii ni theluji, au?
|
|
健太 | これは、粉雪。 粉のようにさらさらしているでしょ。 |
Hii ni theluji ya ungaunga. Ni nyepesi, kavu na laini kama unga, au siyo? |
Kenta | KORE WA, KONAYUKI. KONA NO YÔ NI SARASARA SHITEIRU DESHO. Hii ni theluji ya ungaunga. Ni nyepesi, kavu na laini kama unga, au siyo?
|
|
アンナ | 帰国する前に、雪を見ることができて幸せです。 | Nimefurahi kuona theluji, kabla ya kurejea nchini kwangu.
|
Anna | KIKOKU SURU MAE NI, YUKI O MIRU KOTO GA DEKITE SHIAWASE DESU.
Nimefurahi kuona theluji, kabla ya kurejea nchini kwangu.
|
Vidokezo vya sarufi
NO YÔ NI
NO YÔ NI inamaanisha "kama _".
k.m.) KONA NO YÔ NI (kama ungaunga)
Mwalimu Tufundishe
Umbo la kikamusi + MAE NI
MAE NI (kabla ya) ni kauli ya kusisitiza unachofanya au ulichofanya, kabla ya kufanya kitu kingine. Vitenzi huwa kwenye umbo la kikamusi, ikiwa vitafuatiwa na MAE NI. Hata kama sentensi yote iko katika hali ya wakati uliopita, kitenzi kinachukua umbo la kikamusi kabla ya MAE NI, japo umbo hili linaashiria wakati uliopo.
Tanakali Sauti
Theluji
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Theluji nyepesi inaitwa KONAYUKI. Theluji iliyo majimaji ni BOTANYUKI. Watu husema vipande vikubwa vya theluji vinaonekana kama petali za maua ya BOTAN.
