Somo la 43
Unadhani ni kwa nini?

Anna yupo katika ziara ya kimasomo. Leo amekwenda kwenye kasri la Himeji mkoani Hyôgo.
Usemi wa msingi:
DÔSHITE DESHÔ KA
Mazungumzo
先生 | 姫路城は奇跡の城と言われています。 どうしてでしょうか。 |
Kasri la Himeji linasemekana kuwa ni la ajabu. Unadhani ni kwa nini? |
---|---|---|
Mwalimu | HIMEJI-JÔ WA KISEKI NO SHIRO TO IWARETE IMASU. DÔSHITE DESHÔ KA. Kasri la Himeji linasemekana kuwa ni la ajabu. Unadhani ni kwa nini?
|
|
ロドリゴ | 戦争でも焼けなかったからです。 | Kwa sababu halikuwahi kuunguzwa hata wakati wa vita.
|
Rodrigo | SENSÔ DEMO YAKENAKATTA KARA DESU.
Kwa sababu halikuwahi kuunguzwa hata wakati wa vita.
|
|
アンナ | さすが、ロドリゴ! | Hongera, Rodrigo!
|
Anna | SASUGA, RODORIGO!
Hongera, Rodrigo!
|
Vidokezo vya sarufi
DÔSHITE DESHÔ KA
(Unadhani ni kwa nini?)
DÔSHITE inaamisha "kwa nini." Ili usikike kiungwana, tumia NAZE badala ya DÔSHITE.
k.m.) NAZE DESHÔ KA.
Mwalimu Tufundishe
Namna ya kutumia DESHÔ
Unatumia DESHÔ mwishoni mwa sentensi, unapozungumzia ubashiri wa siku za usoni, au kitu fulani ambacho hakina uhakika.
Tanakali Sauti
Sauti ya jibu sahihi/lisilo sahihi
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kasri la Himeji pia linafahamika kama White Heron. White Heron ni aina fulani ya ndege weupe. Kuna nadharia mbalimbali lakini iliyo maarufu ni kwamba kasri hilo jeupe, linaonekanaka kama ndege huyo.
