NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 42

Somo la 42

Sijui kipi ni kitamu zaidi?

Anna yupo kwenye ziara ya kimasomo. Ananunua kasha la vyakula kwenye treni ya mwendo kasi ya Shinkansen.

Somo la 42 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

DORE GA ICHIBAN OISHII KANA

Mazungumzo

アンナ どれがいちばんおいしいかな。 Sijui kipi ni kitamu zaidi?
Anna DORE GA ICHIBAN OISHII KANA.
Sijui kipi ni kitamu zaidi?
販売員 幕の内弁当は人気がありますよ。 Makunouchi-bento, yaani kasha la vyakula mbalimbali ni maarufu.
Muuzaji MAKUNOUCHI-BENTÔ WA NINKI GA ARIMASU YO.
Makunouchi-bento, yaani kasha la vyakula mbalimbali ni maarufu.
アンナ じゃ、私は幕の内。 Basi, mimi nitachukua Makunouchi.
Anna JA, WATASHI WA MAKUNOUCHI.
Basi, mimi nitachukua Makunouchi.
ロドリゴ 僕も。支払いは別々にお願いします。 Nami pia. Tafadhali tunaomba tulipe mmojammoja.
Rodrigo BOKU MO. SHIHARAI WA BETSUBETSUNI ONEGAI SHIMASU.
Nami pia. Tafadhali tunaomba tulipe mmojammoja.

Vidokezo vya sarufi

DORE GA ICHIBAN   DESU KA

(Kipi ni ... zaidi?)

Ili kuunda swali kwa kutumia ICHIBAN (bora zaidi) unatumia viwakilishi vya kuuliza kabla ya ICHIBAN, kwa kutegemea unachokilinganisha.
Kujifunza zaidi, tafadhali nenda kwenye ukurasa wa "Mwalimu tufundishe".

Mwalimu Tufundishe

ICHIBAN
Unapolinganisha vitu vitatu au zaidi, unaelezea kile kilicho bora kwa kusema ICHIBAN (bora zaidi).

Tanakali Sauti

Njaa
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Stesheni nyingi za treni nchini Japani zina kile kinachofahamika kama EKIBEN, kasha lililo na bidhaa za vyakula vya maeneo husika. Ninataka kula vyakula vilivyo kwenye EKIBEN mbalimbali.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.