Somo la 39
Nafikiri una homa.

Anna hahisi vizuri, na amekwenda hospitalini, akiwa ameambatana na mama msimamizi wa bweni. Sasa anamwona daktari.
Usemi wa msingi:
KAZE DA TO OMOIMASU
Mazungumzo
医者 | どうしましたか。 | Una tatizo gani?
|
---|---|---|
Daktari | DÔ SHIMASHITA KA.
Una tatizo gani?
|
|
アンナ | せきが出ます。 | Nina kikohozi.
|
Anna | SEKI GA DEMASU.
Nina kikohozi.
|
|
寮母 | 熱も37.8度あります。 | Pia ana joto la mwili nyuzi 37.8.
|
Msimamizi wa bweni | NETSU MO SANJÛNANA TEN HACHI DO ARIMASU.
Pia ana joto la mwili nyuzi 37.8.
|
|
医者 | 喉を見せてください。 かぜだと思います。 |
Tafadhali nionyeshe koo lako. Nafikiri una homa. |
Daktari | NODO O MISETE KUDASAI. KAZE DA TO OMOIMASU. Tafadhali nionyeshe koo lako.
Nafikiri una homa.
|
Vidokezo vya sarufi
Dalili
Elezea dalili zako.
ATAMA GA ITAI DESU. (Kichwa kinauma.)
HANAMIZU GA DEMASU. (Nina mafua.)
ONAKA GA ITAI DESU. (Tumbo linauma.)
Mwalimu Tufundishe
Nafikiri kwamba
Unapoelezea fikra, maoni au makisio yako, kwanza unasema kile unachofikiria, na kisha unasema TO OMOIMASU, (Nafikiri kwamba). OMOIMASU ni kitenzi kinachomaanisha (kufikiri). Unaongeza TO baada ya kile unachofikiria.
Tanakali Sauti
kukohoa
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Keshia aliye hospitalini na pia mfamasia waliniambia,
“ODAIJINI” yaani (ugua pole). Kila mmoja alikuwa na wasiwasi kunihusu, na hilo lilinifanya nikaanza kuhisi wananijali. Natumai nitapona haraka iwezekanavyo.
