Somo la 36
Napaswa kusoma.

Baada ya kukaa Shizuoka kwa raha, Anna na Sakura wanarudi Tokyo. Kenta yuko kwenye kituo cha treni kuwasindikiza.
Usemi wa msingi:
BENKYÔ SHINAKEREBA NARIMASEN
Mazungumzo
健太 | 寂しくなります。 | Nitakuwa mpweke.
|
---|---|---|
Kenta | SABISHIKU NARIMASU.
Nitakuwa mpweke.
|
|
アンナ | 私もです。 でも、大学で勉強しなければなりません。 |
Nami pia. Lakini napaswa kusoma katika chuo kikuu changu. |
Anna | WATASHI MO DESU. DEMO, DAIGAKU DE BENKYÔ SHINAKEREBA NARIMASEN. Nami pia. Lakini napaswa kusoma katika chuo kikuu changu.
|
|
健太 | じゃ、僕が春休みに東京に行きます。 | Kisha, nitaenda Tokyo wakati wa mapumziko ya msimu wa chipukizi.
|
Kenta | JA, BOKU GA HARUYASUMI NI TÔKYÔ NI IKIMASU.
Kisha, nitaenda Tokyo wakati wa mapumziko ya msimu wa chipukizi.
|
Vidokezo vya sarufi
Misimu
Tujifunze namna ya kusema misimu minne.
Tafadhali tembelea ukurasa wa "nyenzo za kujifunzia."
Mwalimu Tufundishe
Umbo la NAI la kitenzi + NAKEREBA NARIMASEN
Unaposema ni lazima au unahitajika kufanya jambo fulani, unabadilisha sehemu ya NAI katika kitenzi cha umbo la NAI na kuwa NAKEREBA NARIMASEN.
Tanakali Sauti
Upepo
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kando na likizo ya msimu wa joto, huwa kuna mapumziko shuleni wakati wa msimu wa baridi na chipukizi. Kila msimu una furaha yake, msimu wa majira ya joto watu huenda baharini na msimu wa baridi watu hufanya michezo ya kuteleza kwenye theluji. Bila shaka ni jambo la kufurahisha.
