Somo la 34
Ni laini na mtamu.
Baada ya Anna kuhudhuria tamasha la chuoni na Kenta, wawili hao wamekwenda kwenye mgahawa wa sushi ulio na mkanda wa kubebea chakula.
Usemi wa msingi:
YAWARAKAKUTE OISHII DESU
Mazungumzo
健太 | あっ、トロが来た。 | Oh, toro zimekuja.
|
---|---|---|
Kenta | A', TORO GA KITA.
Oh, toro zimekuja.
|
|
アンナ | トロって何ですか。 | Toro ni nini?
|
Anna | TORO TTE NAN DESU KA.
Toro ni nini?
|
|
健太 | マグロのおなかの部分です。どうぞ。 | Ni mnofu wa sehemu ya tumbo wa samaki tuna. Karibu.
|
Kenta | MAGURO NO ONAKA NO BUBUN DESU. DÔZO.
Ni mnofu wa sehemu ya tumbo wa samaki tuna. Karibu.
|
|
アンナ | いただきます。 やわらかくておいしいです。 |
Nianze kula. Ni laini na mtamu. |
Anna | ITADAKIMASU. YAWARAKAKUTE OISHII DESU. Nianze kula. Ni laini na mtamu.
|
Vidokezo vya sarufi
TTE NAN DESU KA
Unaweza kuuliza ni kitu gani, au maana ya neno kwa kuongeza TTE NAN DESU KA.
k.m.) TORO TTE NAN DESU KA. (Toro ni nini?)
Kivumishi cha umbo la TE + kivumishi
Ikiwa unataka kuelezea kitu kwa kutumia vivumishi viwili au zaidi, unabadilisha kivumishi ama vivumishi vya awali kwenda kwenye umbo la TE.
Ili kujifunza zaidi, tafadhali angalia "Mwalimu Tufundishe."
Mwalimu Tufundishe
Namna ya kutengeneza vivumishi vya umbo la TE.
Ikiwa unataka kuelezea kitu kwa kutumia vivumishi viwili au zaidi, unabadilisha kivumishi ama vivumishi vya awali kwenda kwenye umbo la TE.
Tanakali Sauti
Ladha ya chakula
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Unasema ITADAKIMASU kabla ya kula kushukuru wale waliopika. Pia unashukuru nyama, samaki, mbogamboga pamoja na wale waliokuza na kuvuna mazao hayo.