Somo la 28
Karibu Shizuoka.

Anna amefika mji wa Shizuoka na Sakura. Kenta ambaye ni binamu wa Sakura, yuko katika kituo cha treni ili akutane nao.
Usemi wa msingi:
SHIZUOKA E YÔKOSO
Mazungumzo
さくら | こちらは、いとこの健太くん。 | Huyu ni binamu yangu, Kenta.
|
---|---|---|
Sakura | KOCHIRA WA, ITOKO NO KENTA-KUN.
Huyu ni binamu yangu, Kenta.
|
|
健太 | 静岡へようこそ。 | Karibu Shizuoka.
|
Kenta | SHIZUOKA E YÔKOSO.
Karibu Shizuoka.
|
|
さくら | 彼はカメラに詳しいから、いろいろきいてね。 | Anafahamu mengi kuhusu kamera, kwa hiyo muulize lolote kuhusu kamera.
|
Sakura | KARE WA KAMERA NI KUWASHII KARA, IROIRO KIITE NE.
Anafahamu mengi kuhusu kamera, kwa hiyo muulize lolote kuhusu kamera.
|
|
アンナ | どうぞよろしくお願いします。 | Nitashukuru kwa msaada wako.
|
Anna | DÔZO YOROSHIKU ONEGAI SHIMASU.
Nitashukuru kwa msaada wako.
|
|
健太 | (アンナちゃん、かわいいなあ) | (Anna anapendeza.)
|
Kenta | (ANNA-CHAN, KAWAII NÂ.)
(Anna anapendeza.)
|
Vidokezo vya sarufi
E YÔKOSO
E inaashiria mwisho wa mweleko au eneo la mwisho unakoelekea. YÔKOSO ni "karibu."
k.m.) NIHON E YÔKOSO. (Karibu Japani.)
NI KUWASHII
NI inaonyesha kile ambacho anafahamu.
k.m.) KENTA WA KAMERA NI KUWASHII.
(Kenta anafahamu mengi kuhusu kamera.)
Mwalimu Tufundishe
Tofauti kati ya KARA na NODE
KARA na NODE huelezea sababu. Kwa mfano, ikiwa kivumishi, KAWAII, (kupendeza), ndio sababu, unaweza kusema ama KAWAII KARA au KAWAII NODE.
Tanakali Sauti
king'ora
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Unapozungumzia kuhusu Shizuoka, kitu cha kwanza kinachonijia akilini kwangu ni Mlima Fuji. Ulisajiliwa kama urithi wa dunia mwaka 2013. Nitamuomba Kenta anielezee sehemu nzuri ya kuutazama Mlima Fuji.”
