Somo la 24
Tafadhali msitumie.

Anna anahudhuria darasa la somo la Kijapani ambalo Profesa Suzuki anafundisha. Prof. Suzuki anaelezea juu ya jaribio la wiki ijayo.
Usemi wa msingi:
TSUKAWANAIDE KUDASAI
Mazungumzo
先生 | はい、今日はここまでです。 来週の月曜日に試験をします。 |
Haya, kwa leo tuishie hapa. Jumatatu ijayo nitawapatia jaribio. |
---|---|---|
Mwalimu | HAI, KYÔ WA KOKO MADE DESU. RAISHÛ NO GETSUYÔBI NI SHIKEN O SHIMASU. Haya, kwa leo tuishie hapa.
Jumatatu ijayo nitawapatia jaribio.
|
|
アンナ | 先生、辞書を使ってもいいですか。 | Mwalimu, tunaweza kutumia kamusi?
|
Anna | SENSEI, JISHO O TSUKATTE MO II DESU KA.
Mwalimu, tunaweza kutumia kamusi?
|
|
先生 | いいえ、だめです。使わないでください。 | Hapana, hamruhusiwi. Tafadhali msitumie.
|
Mwalimu | IIE, DAME DESU. TSUKAWANAIDE KUDASAI.
Hapana, hamruhusiwi. Tafadhali msitumie.
|
Vidokezo vya sarufi
Maneno yanayoashiria wakati
Tujifunze maneno ya kuashiria wakati.
Angalia "Nyenzo za kujifunzia."
Mwalimu Tufundishe
Kitenzi cha umbo la NAI + DE KUDASAI
Ikiwa unataka kuwaambia wengine kile ambacho hawaruhusiwi kufanya, unajumuisha vitenzi vya umbo la NAI na DE KUDASAI, na useme NAI DE KUDASAI (Tafadhali usifanye hivyo).
Tanakali Sauti
Kutoridhika
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Juma lijalo, tutakuwa na jaribio. Huwezi kutumia kalamu ya wino. Tumeambiwa tutumie kalamu ya risasi na vifuto. Nitahitajika kuvitayarisha.
