Somo la 21
Hapana, siyo sana.

Katika kibanda cha Karaoke, Anna ameimba wimbo wa Kijapani. Sakura anamsifu Anna kwa uimbaji wake mzuri.
Usemi wa msingi:
IIE, SOREHODODEMO
Mazungumzo
さくら | アンナ、上手だね。 | Anna, unaimba vizuri.
|
---|---|---|
Sakura | ANNA, JÔZU DA NE.
Anna, unaimba vizuri.
|
|
アンナ | いいえ、それほどでも。 | Hapana, siyo sana.
|
Anna | IIE, SOREHODODEMO.
Hapana, siyo sana.
|
|
ロドリゴ | あっ、もうこんな時間です。 | Ah! Muda umekwenda.
|
Rodrigo | A', MÔ KONNA JIKAN DESU.
Ah! Muda umekwenda.
|
|
アンナ | 大変。門限に間に合わない。 | Lo! Sitaweza kuwahi muda wa ukomo wa kurudi.
|
Anna | TAIHEN. MONGEN NI MANIAWANAI.
Lo! Sitaweza kuwahi muda wa ukomo wa kurudi.
|
Vidokezo vya sarufi
IIE, SOREHODODEMO
(Hapana, siyo sana.)
IIE ni jibu la kukanusha. SOREHODODEMO inamaanisha "siyo sana." IIE, SOREHODODEMO ni usemi unaotumiwa ukiwa unataka kuonyesha unyenyekevu au kutokuwa na majivuno.
Mwalimu Tufundishe
Vitenzi vya umbo la NAI
Vitenzi vinavyomalizikia na NAI, vinaitwa "vitenzi vya umbo la NAI."
Tanakali Sauti
Kushangilia
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Nilifikiria Wajapani hawawezi kufurahi hadharani. Lakini sasa ninajua wanapokuwa kwenye mabanda ya Karaoke wanaweza kubadilika. Leo nilihisi tumekuwa marafiki wa karibu.
