Somo la 20
Umewahi kuimba nyimbo za Kijapani?
Anna na wenzake, Sakura na Rodrigo wamefika kwenye kibanda cha Karaoke.
Usemi wa msingi:
NIHON NO UTA O UTATTA KOTO GA ARIMASU KA
Mazungumzo
ロドリゴ | アンナさんは日本の歌を歌ったことがありますか。 | Anna, umewahi kuimba nyimbo za Kijapani?
|
---|---|---|
Rodrigo | ANNA-SAN WA NIHON NO UTA O UTATTA KOTO GA ARIMASU KA.
Anna, umewahi kuimba nyimbo za Kijapani?
|
|
アンナ | はい、あります。 | Ndiyo, nimewahi.
|
Anna | HAI, ARIMASU.
Ndiyo, nimewahi.
|
|
さくら | どんな曲が得意? | Nyimbo gani unazoweza kuimba vizuri?
|
Sakura | DONNA KYOKU GA TOKUI?
Nyimbo gani unazoweza kuimba vizuri?
|
|
アンナ | アニメの曲です。 | Nyimbo za katuni za anime.
|
Anna | ANIME NO KYOKU DESU.
Nyimbo za katuni za anime.
|
Vidokezo vya sarufi
ARIMASU: kitenzi kinachoashiria umilikaji
Katika somo la 7, ARIMASU ilimaanisha “uwepo.” Katika somo la 9, ilimaanisha “kufanyika kwa tukio.”
Sasa, tumejifunza ya kwamba ARIMASU inamaanisha “kuwa na uzoefu” kama vile tajriba.
k.m.) NIHON NO UTA O UTATTA KOTO GA ARIMASU KA.
(Umewahi kuimba nyimbo za Kijapani?)
Mwalimu Tufundishe
Kitenzi cha umbo la TA + KOTO GA ARIMASU
Umbo la TA la vitenzi linaonyesha kitendo kilichofanyika katika wakati uliopita au ambacho kiko katika hali timilifu.
Tanakali Sauti
Treni
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kwa mara ya kwanza nchini Japani nimekwenda katika banda la Karaoke. Nimesikia ya kwamba kuna watu wanaokuja kufanya mazoezi ya kuimba peke yao. Nimeshangaa.