Somo la 19
Ilikuwa vizuri.

Anna alipoteana na rafiki zake na kumpigia simu Sakura ili amusaidie. Je Anna atajumuika tena na Sakura na Rodrigo?
Usemi wa msingi:
YOKATTA
Mazungumzo
ロドリゴ | おーい、アンナさん。 | Anna!
|
---|---|---|
Rodrigo | ÔI, ANNA-SAN.
Anna!
|
|
アンナ | みんな。 | Wote.
|
Anna | MINNA.
Wote.
|
|
ロドリゴ | よかった。心配したよ。 | Ilikuwa vizuri. Tulikuwa na wasiwasi juu yako.
|
Rodrigo | YOKATTA. SHINPAI SHITA YO.
Ilikuwa vizuri. Tulikuwa na wasiwasi juu yako.
|
|
アンナ | ごめんなさい。 カメラが安かったので、つい見てしまいました。 |
Samahani. Kwa sababu kamera zilikuwa bei rahisi, niliangalia tu.
|
Anna | GOMENNASAI. KAMERA GA YASUKATTA NODE, TSUI MITE SHIMAIMASHITA. Samahani. Kwa sababu kamera zilikuwa bei rahisi, niliangalia tu.
|
Vidokezo vya sarufi
Umbo la wakati uliopita la vivumishi
Vivumishi vya Kijapani vina umbo la wakati uliopita. Kwa vivumishi vya I, unabadilisha I ya mwisho kuwa KATTA. Na kwa upande wa vivumishi vya NA, ongeza DATTA.
k.m.)
Kivumishi cha I:
YASUI (bei rahisi)
>> YASUKATTA (ilikuwa bei rahisi)
Kivumishi cha NA:
SUKI (kupenda)
>> SUKIDATTA (nilipenda)
*zingatia:
II (nzuri)
>> YOKATTA (ilikuwa nzuri)
Ili kujifunza zaidi, tafadhali soma "Mwalimu, Tufundishe."
Mwalimu Tufundishe
Umbo la wakati uliopita la vivumishi
Umejifunza ya kwamba kuna aina mbili ya vivumishi kwa Kijapani, yaani vya aina ya I na NA. Vivumishi vya I ni vile ambavyo vinaishia na silabi I, kama vile "rahisi" YASUI. Vivumishi vya NA ni vile ambavyo vinaweka NA mwishoni mwake ili kuvumisha nomino. Mfano ni “kupenda,” SUKI,. Inapovumisha nomino, inageuka na kuwa SUKINA. Kwa hiyo, kitabu cha manga unachokipenda, unasema SUKINA MANGA.
Tanakali Sauti
Kamera
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Nilipotea njia. Sakura na Rodrigo wakawa na wasiwasi juu yangu. Samahani kwa hilo. Lakini nilipokuwa nikiwasubiri, nilinunua kamera. Je, nitapiga picha za aina gani kwa kutumia kamera hiyo?
