Somo la 14
Naweza kutupa taka hapa?

Anna anafanya usafi baada ya karamu iliyofanyika katika bweni lao.
Usemi wa msingi:
KOKO NI GOMI O SUTETE MO IIDESU KA
Mazungumzo
アンナ | お母さん、ここにゴミを捨ててもいいですか。 | Mama, naweza kutupa takataka hapa?
|
---|---|---|
Anna | OKÂSAN, KOKO NI GOMI O SUTETE MO II DESU KA.
Mama, naweza kutupa takataka hapa?
|
|
寮母 | そうねえ。缶は別の袋に入れてください。資源ですから。 | Aha. Tafadhali weka makopo kwenye mfuko mwingine.
Kwa sababu ni rasilimali.
|
Msimamizi wa bweni | SÔNÊ. KAN WA BETSU NO FUKURO NI IRETE KUDASAI. SHIGEN DESU KARA.
Aha. Tafadhali weka makopo kwenye mfuko mwingine.
Kwa sababu ni rasilimali.
|
|
アンナ | はい、分かりました。 | Naam, nimeelewa.
|
Anna | HAI, WAKARIMASHITA.
Naam, nimeelewa.
|
Vidokezo vya sarufi
KARA
Katika muktadha huu, KARA inaonyesha sababu.
k.m.) SHIGEN DESU KARA, BETSU NO FUKURO NI IRETE KUDASAI. (Kwa sababu hizo ni rasilimali, tafadhali uziweke kwenye mfuko mwingine.)
Mwalimu Tufundishe
Kitenzi cha umbo la TE + MO II DESU KA
Ikiwa kitenzi cha umbo la TE na MO II DESU zinatamkwa kwa pamoja, inamaanisha ya kwamba ombi la ruhusa limekubaliwa.
Tanakali Sauti
Kuchoma
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kuna masharti ya kina kuhusiana na suala la kutenganisha takataka. Ni lazima tuoshe makopo na chupa za plastiki kabla ya kuzitupa. Nitajitahidi, kadiri ya uwezo wangu.
