Somo la 10
Je, wote wapo?

Leo, Anna atafanyiwa uchunguzi wa afya katika chuo chake. Wanafunzi wamekusanyika katika eneo la kufanyiwa uchunguzi.
Usemi wa msingi:
ZEN-IN IMASU KA
Mazungumzo
先生 | はじめに身長と体重をはかります。 全員いますか。 |
Kwanza, tutapima urefu na uzito
wenu. Je, wote wapo?
|
---|---|---|
Mwalimu | HAJIMENI SHINCHÔ TO TAIJÛ O HAKARIMASU. ZEN-IN IMASU KA. Kwanza, tutapima urefu na uzito
wenu. Je, wote wapo?
|
|
ロドリゴ | アンナさんがいません。 | Anna hayupo.
|
Rodrigo | ANNA-SAN GA IMASEN.
Anna hayupo.
|
|
アンナ | すみません。遅れました。 | Samahani. Nimechelewa.
|
Anna | SUMIMASEN. OKUREMASHITA.
Samahani. Nimechelewa.
|
Vidokezo vya sarufi
MASHITA: Umbo la wakati uliopita la MASU
Namna ya kugeuza kitenzi cha umbo la MASU kuwa katika umbo la wakati uliopita, unabadilisha MASU kuwa MASHITA.
k.m. )TABEMASU (kula) >> TABEMASHITA (nilikula)
Mwalimu Tufundishe
IMASU na ARIMASU
Katika somo la 7, Anna alishangaa alipoona keki nyingi kwenye duka la kuuza keki, na akasema KÊKI GA IPPAI ARIMASU (Kuna keki nyingi). Katika muktadha huu, ikiwa kiima kinahusu vitu visivyo na uhai, unatumia ARIMASU.
Tanakali Sauti
Kukatishwa tamaa
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Leo nimechelewa kidogo tu. Lakini nimesikia nchini Japani, wale wanaochelewa katika mikutano hawaaminiki. GÂN.
