Somo la 1
Mimi ni Anna.

Anna ni mwanafunzi kutoka Thailand. Leo anakutana na mwelekezi wake Sakura kwa mara ya kwanza katika chuo kikuu.
Usemi wa msingi:
WATASHI WA ANNA DESU
Mazungumzo
アンナ | はじめまして。私はアンナです。 | Nashukuru kukutana nawe. Mimi ni Anna. |
---|---|---|
Anna | HAJIMEMASHITE. WATASHI WA ANNA DESU. Nashukuru kukutana nawe. Mimi ni Anna.
|
|
さくら | はじめまして。さくらです。 | Nami pia. Mimi ni Sakura. |
Sakura | HAJIMEMASHITE. SAKURA DESU. Nami pia. Mimi ni Sakura.
|
|
アンナ | よろしくお願いします。 | Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa.
|
Anna | YOROSHIKU ONEGAI SHIMASU.
Tuendelee kuwa na uhusiano mwema kuanzia sasa.
|
|
さくら | こちらこそ。 | Ni mimi ninayestahili kusema hivyo.
|
Sakura | KOCHIRAKOSO.
Ni mimi ninayestahili kusema hivyo.
|
Vidokezo vya sarufi
A WA B DESU
(A ni B.)
WA inaonyesha mada.
B na DESU kwa pamoja zinakuwa taarifa juu ya kiima.
k.m.) WATASHI WA ANNA DESU. (Mimi ni Anna.)
Herufi za Kijapani
Lugha ya Kijapani ina aina tatu ya mfumo wa herufi:
Hiragana, Katakana na Kanji, kila moja ikiwa na jukumu lake.
Mwalimu Tufundishe
Mfumo wa uandishi wa Kijapani
Lugha ya Kijapani ina aina tatu ya mfumo wa herufi, kila moja ikiwa na jukumu lake. Unapoandika WATASHI WA ANNA DESU (Mimi ni Anna), nomino ya kujitambulisha yaani "mimi," WATASHI, inaandikwa kwa herufi ya Kanji.
Tanakali Sauti
PON
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Nchini Japani watu wanaposalimiana, huinamisha kichwa. Ni nadra sana kusalimiana kwa kupeana mkono. Ni kama ilivyo Thailand.
