NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Jinsi ya kutumia podcasting

Jinsi ya kutumia podcasting

"Jifunze Kijapani" kwa podcasting

NHK WORLD RADIO JAPAN inatoa masomo ya "Jifunze Kijapani" yaliyohifadhiwa kwenye mfumo wa sauti kwa kutumia njia ya podcasting. Ukisajiliwa mara moja, kila wakati somo litakapowekwa kwenye tovuti, litakuwa linajipakua lenyewe kwenye kifaa unachotumia. Unaweza kusikiliza sauti iliyopakuliwa hata kwenye maeneo ambayo hayana mtandao. Huna haja ya kuwa na wasiwasi wa kukosa toleo la somo jipya.

Ili uweze kutumia huduma hii

Ili uweze kutumia huduma hii, programu na mtandao ni lazima. Programu za kuwezesha huduma ya podcasting zinapatikana kupitia mtandaoni.

Upande wa smartphone na tarakilishi ndogo:

 1. Pakua programu kutoka kwa podcasting hadi kwenye kifaa chako.
 2. Fungua programu, na utafute "Jifunze Kijapani" ya NHK WORLD.
 3. Chagua "Jifunze Kijapani" na uisajili.

Ikiwa unatumia tarakilishi binafsi:

iTunes
 1. Pakua na uweke progaramu ya podcasting kama vile iTunes na kadhalika kwenye tarakilishi yako.
 2. Sajili somo unalotaka kusikiliza kwenye programu
  (Ikiwa unatumia iTunes)
  Anzisha program hiyo, na uchague "Podcast" kutoka kwenye menyu.
  Fungua ukurasa wa "Jifunze Kijapani", buruta na udondoshe alama iliyoandikwa "RSS Podcasting" kwenye skrini ya iTunes. Mchakato huo utakuwa umekamilika.