はるさんハウスはどこですか Nyumba ya Haru-san iko wapi?
タムです。学生です Mimi ni Tam. Ni mwanafunzi.
ベトナムから来ました Ninatokea Vietnamu.
大学で日本語を勉強します Nitasoma Kijapani katika chuo kikuu.
ラジオで勉強しました Nimejifunza kwa kusikiliza redio.
この電車は池袋に行きますか Treni hii inakwenda Ikebukuro?
ゆっくり話してください Tafadhali zungumza polepole.
友達のあやかさんです Huyu ni rafiki yangu, Ayaka-san.
これは何ですか Hii ni nini?
このドライヤーはいくらですか Hiki kikausha nywele ni bei gani?
お守りはありますか Kuna hirizi za bahati?
かわいいお守りですね Hii ni hirizi nzuri, sivyo?
雪が見たいです Nataka kutazama theluji.
日本へ行ってみたいです Ningependa kwenda Japani.
猿の温泉までお願いします Naelekea chemchemi ya majimoto ya nyani tafadhali.
有名な温泉です Hii ni chemchemi maarufu ya majimoto.
日本を旅行しています Nimekuwa nikisafiri sehemu mbalimbali Japani.
すごく楽しかったです Kulifurahisha kweli.
手袋が欲しいんですが Nahitaji jozi ya glavu.
わさびは入れないでください Tafadhali usiweke kiungo cha wasabi.
時計台の中にいます Nipo ndani ya mnara wa saa.
写真を撮りましょう Tupige picha.
私はこの猫が好きです Mimi nampenda paka huyu.
生卵は食べられません Siwezi kula mayai mabichi.
のどが痛いんです Koo langu linauma.
この卵焼き、甘くておいしいです Hiki kimanda cha Kijapani ni kitamu na kina ladha nzuri.
どれが一番おいしいですか Kipi ni kitamu zaidi?
写真を撮ってもいいですか Ninaweza kupiga picha?
ピアノの演奏を聴きに行きました Nilikwenda kusikiliza onyesho la piano.
一緒に歌ったり、踊ったりしました Tuliimba nyimbo na kucheza dansi pamoja.
一緒に行きませんか Kwa nini tusiende pamoja?
忍者博物館まで、どう行ったらいいですか Nawezaje kufika Makumbusho ya Ninja?
どのくらい待ちますか Nitasubiri kwa muda gani?
読んだことあります Nimewahi kukisoma.
大涌谷に行って、黒たまごが食べたいです Ninataka kwenda Owakudani na kula mayai meusi.
お風呂は何時から何時までですか Tunaweza kutumia bafu kuanzia saa ngapi hadi saa ngapi?
テレビがつかないんですが・・・ Runinga haiwaki…
外のほうがいいです Nje ni bora.
財布を落としてしまいました Nimepoteza pochi yangu.
初めてだったから、びっくりしました Kwa kuwa ilikuwa ni mara yangu ya kwanza, nimeshtuka.
チケットを買うことができますか Tunaweza kununua tiketi?
悠輝さんに渡すつもりです Ninadhamiria kumpatia Yuuki-san.
元気そうですね Unaonekana mwenye afya.
またコンサートがあるそうです Nimesikia onyesho lingine litafanyika.
日本語をチェックしてもらえませんか Unaweza kuangalia usahihi wa Kijapani?
小さいけどきれいですね Ni ndogo lakini inapendeza.
どうやってするんですか Unafanyaje?
卒業したら、日本で働きたいです Nikihitimu, nataka kufanya kazi nchini Japani.