Tutajibu Maswali Yenu

Wasimamizi wa kipindi Fujinaga Kaoru na Isomura Kazuhiro wanajibu maswali ya wasikilizaji kuhusu lugha ya Kijapani.

Q1 Naipenda Japani na utamaduni wake. Kwa kutazama katuni za anime nimeelewa Kijapani cha msingi. Ningependa kujifunza mwenyewe lugha hii. Nadhani "Jifunze Kijapani" itanisaidia, lakini sijui jinsi ya kusoma kwa ufasaha.

Ni vizuri kwamba amejifunza Kijapani cha msingi kwa kutazama anime! Kwa kutazama visa mbalimbali vya katuni ameweza kufahamu maneno na semi zinazohusiana na hali husika. Katika kujifunza lugha ni muhimu kutazama na kusikiliza tukio, kufahamu maana ya maneno na matumizi yake, kutambua semi zitakazokuwa za msingi kwako na kisha kuzitumia.

"Jifunze Kijapani" ni kwa ajili ya watu wanaotaka kujifunza wenyewe. Kwa kufuatilia kipindi sambamba na maandishi kidogo kidogo utaweza kuelewa na kujifunza namna ya kuongea Kijapani cha msingi.

Kwanza sikiliza mazungumzo katika kila somo. Baadhi ya maneno na semi zinaweza kuwa mpya kwako lakini hakuna haja ya kuwa na wasiwasi juu ya vitu vidogo kwanza. Ikiwa unaweza kuelewa simulizi yote kwa kusoma tafsiri ya mazungumzo na maelezo juu ya simulizi basi inatosha.

Halafu soma au sikiliza maelezo yanayotolewa katika kipengele cha "Usemi wa Msingi." Kila usemi wa msingi ni muhimu kwa kinachofundishwa kwenye somo.

Kisha kipengele cha "Tumia!" kinakupa mwanya wa kufanyia mazoezi semi katika hali husika unazoweza kukutana nazo Japani. Zingatia matamshi yako na rudia semi kwa sauti mara kadhaa.

Kipengele cha "Jaribu!" kinakupa fursa ya kutumia usemi wa msingi. Ikiwa unasikiliza kipindi au unajifunza kupitia tovuti unaweza kuangalia majibu kwenye maandishi na sauti. Hivyo unaweza kufanya mazoezi mwenyewe.

Masomo yanajumuisha kipengele cha "Usemi wa Ziada" kinachokupatia semi unazoweza kutumia kama zilivyo na taarifa za nyongeza kuhusu Japani zinazohusiana na kila mzungumzo ya somo.

Unaweza kusikiliza sauti kwenye tovuti mara nyingi upendavyo. Hivyo unaweza kujifunza kwa kasi yako kidogo kidogo, hatua kwa hatua.

Q2 Kuna tofauti gani kati ya Hiragana, Katakana na Kanji? Ipi nijifunze kwanza?

Hiragana na Katakana ni herufi zinazoelezea sauti mbalimbali. Mfano ili kuelezea sauti " a", tunatumia "" ya Hiragana, au "" ya Katakana.

Kwa upande mweingine, herufi za Kanji zinaelezea maana. Ni kama tu emoji ya kutabasamu, Kanji huelezea maana. Mfano, "kimasu" inaweza kumaanisha "kuja" au "kuvaa" kwa Kijapani. Ikiandikwa kwa Hiragana, zote ni sawa, ila ikiandikwa kwa Kanji, "来ます" "着ます", tunaweza kutofautisha kwa urahisi.

Kwa kawaida tunaandika Kijapani kwa Kanji na Hiragana. Tunatumia Kanji katika sehemu zinazoelezea maana, kama nomino na vitenzi. Halafu Hiragana katika sehemu zingine. Hata hivyo tunapoandika maneno yenye asili ya lugha zingine tunatumia Katakana. Maneno kama "コーヒー koohii" yaani kahawa, au majina kama "タム Tamu" Tam ya watu kutoka nchi zingine. Pia majina ya nchi kama "ベトナム Betonamu" yaani Vietnamu huandikwa kwa Katakana.

Unapojaribu kukariri herufi, kuanza na Hiragana na Katakana pengine ni njia nzuri. Kisha hamia kwenye Kanji. Hiyo ni kwa sababu utaweza kuandika Kijapani rahisi katika Hiragana na Katakana. Nadhani ni bora kujifunza Kanji kidogo kidogo.

Q3 Unaandikaje Kanji kwenye kompyuta au simu?

Watu wengi hutumia modi ya alfabeti za kirumi, kuingiza herufi za Kijapani wakati wanapoandika Kijapani kwenye kibodi.

Mfano ukitaka kuandika "kawa" -yaani mto - katika Kanji, kwanza unaandika "k" "a" "w" "a." Programu ya kompyuta itabadili herufi hizo kuwa "kawa" katika Hiragana,"かわ." Kisha itakuonesha orodha ya Kanji zinazofanania na unachotaka kuandika kama vile "" ngozi, au "" mto. Utachagua Kanji sahihi unayotaka kutumia, kwa hapa Kanji ya mto, itakuwa "."

Kwenye simu unaweza kutumia modi ya alfabeti za kirumi au unaweza kutumia kibodi mpapaso. Kibodi mpapaso inakuwezesha kuandika Hiragana moja kwa moja kwa kutelezesha kidole chako kwenye skrini ya kugusa. Machaguo ya Kanji ya kubadili Hiragana yatakuja kama tu kwenye kibodi ya kompyuta.

Q4 Katika somo la 6, nimejifunza namba kwa Kijapani. Lakini zilitamkwa tofauti kidogo na nilivyojifunza kwenye sanaa ya mapigano ya Budo. Namba 4 ilitamkwa "shi" badala ya "yon." Namba 7 ilitamkwa "shichi" badala ya "nana." Kuna tofauti gani?

Katika Kijapani, kuna namna mbili za kuhesabu. "Hitotsu・futatsu・mittsu・yottsu・itsutsu・muttsu・nanatsu・yattsu…" ni namna Wajapani walivyohesabu tangu enzi za kale. "Ichi・ni・san・shi・go・roku・shichi・hachi…" ni matamshi ya namba yenye asili ya China.

Katika "Jifunze Kijapani" tumetambulisha "ichi・ni・san・yon・go・roku・nana・hachi…." 4 inatamkwa "yon," sio "shi." Na 7 inatamkwa "nana," sio "shichi." "Yon" imetokana na "yottsu" katika namna ya kuhesabu ya kizamani ya Kijapani, na "nana" inatokana na "nanatsu."

Hivyo ndivyo unavyosema kwa kawaida unapotumia namba yenyewe au kusema kuna vitu vingapi.

Hata hivyo katika hali kama sanaa ya mapigano, ambapo mijongeo na mambo mengine yanahesabiwa kwa mfuatano: "ichi・ni・san・shi・go・roku・shichi・hachi…."

Utofauti kwa kawaida huamuliwa. Hivyo unatakiwa kukariri unapokutana nazo. Mfano, kwa yeni 400 unatakiwa kutumia "yon" na useme "yon-hyaku-en." Kwa ¥4,000, sema "yon-sen-en." Na kwa mwezi wa Nne, tumia "shi" na useme "shi-gatsu." "Nana" hutumika kwa ¥700, "nana-hyaku-en." ¥7,000 ni "nana-sen-en." Lakini mwezi wa Saba hutamkwa "shichi-gatsu."

Q5 Kwa kawaida "dakika" hutamkwa "ふん fun," lakini ikiwa na namba zingine huwa "ぷん pun." Inachanganya. Kuna kanuni yoyote ya kufuata?

Kimsingi "dakika" husomwa kama "ふん fun," lakini katika hali fulani herufi f ya kwenye "ふん fun" hubadilika kuwa herufi p na hivyo inakuwa "ぷん pun." Hi ni kutokana na utamaduni wa zamani ambapo "ha hi fu he ho" zilikuwa zikitamkwa "pa pi pu pe po."

Basi, tunaweza kukumbuka ni wakati gani wa kutumia "ぷん pun." Dakika hutamkwa "ぷん pun" ikiwa namba inayokuwa kabla ni 1・3・6・8, au 10. Hivyo ni, "ippun," "sanpun," "roppun," "happun," na "juppun."

Hata hivyo baadhi ya watu hutamka "dakika 4" kama "yonpun" na "dakika 8" kama "hachifun."

Kwa ujumla, namba inayokuja kabla ya dakika huamua sauti. Vivyo hivyo katika neno kama "hon," linalotumika kuhesabu vitu virefu kama mwavuli na kalamu. Hii inaweza kusikika ni usumbufu na ya kuchanganya, ila unaweza kujifunza kwa usahihi kidogo kidogo.

Q6 Ukitaka kumuuliza mtu ana watoto wangapi, vipi ni sahihi: "Kodomo wa nan-nin arimasu ka" au "Kodomo wa nan-nin imasu ka"? Tafadhali elezea tofauti ya "arimasu" na "imasu."

Tunatumia "imasu" kwa viumbe hai "vinavyojongea" kama watu na wanyama. "Arimasu" hutumika kwa vitu.

Kwa mfano, katika somo la 21, tulijifunza usemi wa "Tokeedai no naka ni imasu" yaani, "Nipo ndani ya mnara wa saa." Somo la 11 lilikuwa na usemi "Omamori wa arimasu ka": "Kuna hirizi za bahati?" Kwa hiyo, ukitaka kuuliza "Una watoto wangapi?" tumia "imasu" na useme, "Kodomo wa nan-nin imasu ka."

Ni kweli kwamba zamani, "arimasu" wakati mwingine ilitumika kurejelea wanafamilia na wengine. Unaweza kukutana nayo bado katika sentensi za mfano katika vitabu vya kiada vya zamani. Lakini siku hizi sanifu ni "imasu."

Tuangalie mfano mwingine: "Kuna samaki kwenye bwawa." unasema, "Ike ni sakana ga imasu." Unatumia "imasu" kwa sababu samaki wana uhai na wanajongea. Kwa upande mwingine ukitaka kusema, "Kuna samaki kwenye friji," "Reezooko ni sakana ga arimasu," neno sahihi ni "arimasu" kwa sababu samaki hawajongei tena.