NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Umbo la TE la kitenzi + KARA (Somo la 44)

Mwalimu Tufundishe

Umbo la TE la kitenzi + KARA (Somo la 44)

Katika somo la 16, ulijifunza kwamba unaweza kuelezea zaidi ya tukio moja kwenye sentensi moja kwa kuunganisha vitenzi vya umbo la TE.
Ikiwa utaongeza KARA, baada ya vitenzi vya umbo la TE, unaweza kuweka bayana kwamba, kitendo kilichojitokeza kabla ya KARA kinatangulia kitendo kinachofuata baada ya neno hilo. Kwa namna hii unaweza kusisitiza mpangilio wa vitendo. Katika mazungumzo ya somo la leo, ni muhimu uanze kwa kula kitamutamu cha Kijapani, WAGASHI O TABEMASU, kisha, “unywe chai ya kijani,” MACCHA O NOMIMASU.
Hivyo kitenzi cha kwanza kimekuwa katika umbo la TE na kufuatiwa na KARA, yaani, WAGASHI O TABETE KARA, MACCHA O NOMIMASU, (Baada ya kula vitamutamu vya Kijapani, unakunywa chai ya kijani).

Unaweza pia kutumia KARA, unapojibu swali.
Kwa mfano ukiulizwa, “Utakula chakula cha mchana saa ngapi?” na ukajibu, “baada ya kumaliza kusoma." "Kusoma" ni BENKYÔ. “Kumalizika" ni OWARIMASU. Umbo lake la TE ni OWATTE. Na "kula" ni TABEMASU. Kwa hiyo unasema, BENKYÔ GA OWATTE KARA TABEMASU.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.