NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Namna ya kutumia DESHÔ (Somo la 43)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kutumia DESHÔ (Somo la 43)

Unatumia DESHÔ mwishoni mwa sentensi, unapozungumzia ubashiri wa siku za usoni, au kitu fulani ambacho hakina uhakika.

Unapolisema pamoja na nomino au vivumishi, unabadilisha DESU mwisho wa sentensi kuwa DESHÔ. Tujaribu katika sentensi isemayo “Kesho mvua itanyesha.” "Kesho" ni ASHITA. “Mvua” ni AME. “Kesho kutanyesha” ni ASHITA WA AME DESU. Ikiwa utabadilisha DESU na kuwa DESHÔ, sentensi hiyo itakuwa ASHITA WA AME DESHÔ (Huenda kesho mvua itanyesha).

Ikiwa utatumia pamoja na vitenzi, unabadilisha vitenzi katika muundo wa kawaida kama vile umbo la kikamusi au umbo la NAI na uongeze DESHÔ. Tujaribu sentensi isemayo “huenda atakwenda.” Kwanza tuzingatie “atakwenda.” Katika muktadha huu anayekwenda ni mwanaume, na kinatumika kiwakilishi cha KARE. “Kwenda” ni IKIMASU. Kwa hiyo unasema KARE WA IKIMASU. Sasa, umbo la kikamusi la IKIMASU ni IKU. Kwa hiyo, “huenda atakwenda” ni KARE WA IKU DESHÔ.

Katika somo la 25, umejifunza YÔ DA (inaonekana). Namna ya kiungwana ni YÔ DESU. Inafanana na DESHÔ. Lakini tofauti iko wapi?
Tulinganishe mifano ifuatayo.

KARE WA IKU YÔ DESU ni "inaonekana atakwenda."
KARE WA IKU DESHÔ ni "nadhani atakwenda."
Kama inavyojitokeza wazi hapo juu, unatumia YÔ DESU au YÔ DA, ikiwa unadhani atakwenda, kulingana na hali ilivyo.
Unatumia DESHÔ, unapobashiri tu kile amabcho kitatokea katika siku za usoni.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.