NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > ICHIBAN (Somo la 42)

Mwalimu Tufundishe

ICHIBAN (Somo la 42)

Unapolinganisha vitu vitatu au zaidi, unaelezea kile kilicho bora kwa kusema ICHIBAN (bora zaidi).
Kwa mfano ikiwa unataka kusema, kitu fulani kinafurahisha zaidi, unasemaje? Kinafurahisha ni OMOSHIROI. Hivyo unasema ICHIBAN OMOSHIROI DESU. Kivumishi OMOSHIROI hakibadiliki.
Unaeleza wigo wa mlinganisho kwa DE. “Namba moja katika Japani” ni NIHON DE ICHIBAN. Kama unataka kusema "mlima Fuji ndio mrefu zaidi nchini Japani" unasemaje?”
“Mrefu” ni TAKAI. Hivyo unasema FUJISAN WA NIHON DE ICHIBAN TAKAI DESU. Hebu tutunge sentensi yenye swali kwa kutumia ICHIBAN (cha kwanza, au kilicho bora zaidi). Unatumia viwakilishi vya kuuliza kabla ya ICHIBAN, kwa kutegemea unachokilinganisha.

Ikiwa unalinganisha vitu vilivyo mbele yako, unatumia DORE GA (ipi). Mfano, "ni kipi unachopenda zaidi?” “Kupenda” ni SUKI. Hivyo unasema DORE GA ICHIBAN SUKI DESU KA.
Ikiwa utalinganisha vitu ambavyo haviko mbele yako, unatumia NANI GA (nini). Kwa hiyo, "ni kipi unachokipenda zaidi?” ni NANI GA ICHIBAN SUKI DESU KA.
Ikiwa unalinganisha watu, unatumia DARE GA (nani).
Ikiwa unalinganisha mahali, unatumia DOKO GA (wapi). Ikiwa unalinganisha tarehe, unatumia ITSU GA (lini).
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.