NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Tofauti kati ya AGEMASU na KUREMASU (Somo la 33)

Mwalimu Tufundishe

Tofauti kati ya AGEMASU na KUREMASU (Somo la 33)

katika Kijapani vitenzi tofauti hutumika, kutegemea mtazamo wa mtoaji au mpokeaji.

Kama vile Kenta kwenye mazungumzo ya leo, wakati mzungumzaji anapompatia kitu msikilizaji, anatumia AGEMASU (ninakupatia). AGEMASU pia hutumika wakati watu wanapompatia mwingine kitu fulani. Lakini hapa uwe makini. Ukitumia AGEMASU unapompatia mkuu wako kitu, halitakuwa jambo la kiungwana.
Katika muktadha kama huo, utumie SASHIAGEMASU, badala ya AGEMASU.
SASHIAGEMASU ni kauli inayoashiria heshima kwa anayepokea kitu.

Kwa upande mwingine, ikiwa mtu fulani atakupatia kitu, tumia neno KUREMASU (kunipatia).
Kwa hiyo, Kenta atakapompa Anna picha, Anna atatumia neno KUREMASU.
Pia unatumia KUREMASU, ikiwa mtu uliye karibu naye, kama vile mtu wa familia, atapewa kitu na mwingine. Wale ulio karibu nao unawaita UCHI.

Tofauti kati ya UCHI, (watu walio karibu na wewe), na SOTO, (watu walio na uhusiano wa mbali na wewe), ni muhimu katika mazungumzo ya Kijapani. Utatumia maneno ya kawaida, unapozungumzia watu walio na uhusiano wa karibu na wewe yaani UCHI.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.