NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Tofauti kati ya TARA na TO (Somo la 30)

Mwalimu Tufundishe

Tofauti kati ya TARA na TO (Somo la 30)

TARA na TO zote mbili zinaonyesha sharti. Ikiwa kitu kitatokea kutokana na sharti fulani, unatumia TARA au TO kuashiria sharti hilo.

Lakini utumiaji wa TO unakuwa wa kiwango kidogo kulinganisha na wa TARA. TO, unatumia unapoashiria ya kwamba katika sharti fulani, kuna kitu ambacho lazima kitokee, kiwe ni sheria ya maumbile au desturi, n.k. Kwa mfano, unapotaka kusema, “Ikiwa utabonyeza swichi, taa itawaka.” Hapa, TO inaunganisha sharti, “unabonyeza swichi,” OSHIMASU, na matokeo yake, “taa itawaka,” TSUKIMASU. Kwa hiyo unapotumia TO, unasema OSU TO TSUKIMASU. Katika muktadha huu, pia unaweza kutumia TARA, na ukasema OSHITARA TSUKIMASU. Kwa upande mwingine, huwezi kutumia TO, ikiwa unaelezea nia yako baada ya kuonyesha sharti fulani.
Pia utahitajika kutumia TARA , unapomualika mtu kufanya jambo fulani, au unapoelelezea ombi ama matumaini. Kwa hiyo unatumia TARA kwenye sentensi kama vile AME GA FUTTARA, KAERIMASHÔ, (Ikiwa kutanyesha, turudi).
TARA inaweza kutumiwa kwenye aina nyingi ya muktadha ukilinganisha na TO. Kwa hiyo, ikiwa huna uhakika ni ipi itakayokufaa zaidi, ni vizuri utumie TARA.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.