NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Namna ya kutamka tarehe (Somo la 27)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kutamka tarehe (Somo la 27)

Kwa Kijapani, tarehe mosi ni TSUITACHI.
Awali, neno hilo lilikuwa linamaanisha siku ambayo mwezi huandama. Kuanzia tarehe mbili hadi kumi, unazitamka kama ifuatavyo.

tarehe 2 : FUTSUKA
tarehe 3 : MIKKA
tarehe 4 : YOKKA
tarehe 5 : ITSUKA
tarehe 6 : MUIKA
tarehe 7 : NANOKA
tarehe 8 : YÔKA
tarehe 9 : KOKONOKA
tarehe 10 : TÔKA

Kama ulivyojifunza katika somo la 7, maneno hayo yanatokana na namna ya zamani ya kuhesabu namba kwa Kijapani.

Kuanzia tarehe 11 hadi mwisho wa mwezi, unatamka namba kwa namna ya kawaida kwa kuongeza NICHI, ambayo inamaanisha “tarehe au siku.” Kwa mfano, “tarehe 11” ni JÛICHINICHI.

Lakini kuna siku tatu ambazo hazifuati kanuni hiyo. “Tarehe 14” ambayo ni JÛYOKKA, “tarehe 20” ambayo ni HATSUKA, na tarehe 24 ambayo ni NIJÛYOKKA.

Tafadhali nenda kwenye "Nyenzo za kujifunzia."
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.