NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Kitenzi cha umbo la TA + KOTO GA ARIMASU (Somo la 20)

Mwalimu Tufundishe

Kitenzi cha umbo la TA + KOTO GA ARIMASU (Somo la 20)

Umbo la TA la vitenzi linaonyesha kitendo kilichofanyika katika wakati uliopita au ambacho kiko katika hali timilifu.
Hayo ndio ambayo umejifunza katika masomo yaliotangulia.
Na ikiwa utaunganisha umbo la TA la kitenzi na KOTO GA ARIMASU, unaweza kuzungumzia kitu ambacho umekifanya katika siku za nyuma yaani tajriba ulionayo.

Kwa mfano ikiwa utabadilisha UTAIMASU (kuimba) na kuwa UTATTA KOTO GA ARIMASU, utasema "Nimewahi kuimba au nina tajriba ya kuimba." Ili ubadilishe ARIMASU kuwa umbo la kukanusha, unasema ARIMASEN. Kwa hiyo, umbo la kukanusha la UTATTA KOTO GA ARIMASU (Nimewahi kuimba) ni UTATTA KOTO GA ARIMASEN (Sijawahi kuimba).

Unahitajika kuwa muangalifu kuhusiana na jambo moja.
Huwezi kutumia namna hii ya kuelezea tajriba, yaani kuunganisha umbo la TA la vitenzi na KOTO GA ARIMASU pamoja na maneno yanayoonyesha wakati wa hivi karibuni, kama vile KINÔ (jana), au SENSHÛ (juma lililopita). Katika muktadha kama huo, unahitajika kutumia vitenzi vya umbo la wakati uliopita.

Kwa mfano, ikiwa umeulizwa, “Je, umewahi kuuona Mlima Fuji?” Ikiwa uliuona juma lililopita, huwezi kusema SENSHÛ MITAKOTO GA ARIMASU (Nimewahi kuuona juma liliyopita). Unahitajika kutumia umbo la wakati uliopita la MIMASU (kuona), yaani MIMASHITA (niliona), na kusema SENSHÛ MIMASHITA, (Niliuona wiki iliyopita). 
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.