Mwalimu Tufundishe
Namna ya kuuliza maswali (Somo la 2)
Unapouliza maswali kwa Kijapani, hubadilishi mpangilo wa maneno. Unachofanya ni kuongeza kitamkwa, KA mwisho wa sentensi na kusema kwa toni ya juu.Kwa hiyo, KORE WA OMIYAGE DESU (Hii ni zawadi), ukitaka iwe swali, inakuwa KORE WA OMIYAGE DESU KA (Je hii ni zawadi?)
Sasa, tutafautishe tena sentensi ya kawaida na ile ya swali.
KORE WA OMIYAGE DESU. (Hii ni zawadi.)
KORE WA OMIYAGE DESU KA. (Je hii ni zawadi?)

