NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Mwalimu Tufundishe > Kitenzi cha umbo la TE + SHIMAIMASHITA (Somo la 18)

Mwalimu Tufundishe

Kitenzi cha umbo la TE + SHIMAIMASHITA (Somo la 18)

Ukisema SHIMAIMASHITA baada ya kitenzi cha umbo la TE, unasema ya kwamba umemaliza au umekamilisha jambo ulilokuwa ukifanya, na huwezi kulirejesha katika hali yake ya awali. Kwa hiyo mara nyingi unatumia SHIMAIMASHITA, ikiwa umekosea kufanya jambo fulani na unajutia. Kwa mfano, umevunja sahani. “Kuvunja” ni WARIMASU. Katika neno hili, silabi iliyopo kabla ya MASU ni RI. Kwa hiyo umbo la TE la kitenzi cha WARIMASU ni WATTE. Katika neno hili unaongeza SHIMAIMASHITA. WATTE SHIMAIMASHITA inamaanisha "Nimevunja sahani." Kwa namna hii, umeonyesha ya kwamba umevunja sahani kwa kutokuwa muangalifu.
*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.