NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 9

Somo la 9

Kuanzia saa ngapi?

Leo, Profesa Suzuki atatoa tangazo darasani. 

Somo la 9 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

NANJI KARA DESU KA

Mazungumzo

先生 明日、健康診断があります。 Kesho, kuna uchunguzi wa afya.
Mwalimu ASHITA, KENKÔSHINDAN GA ARIMASU.
Kesho, kuna uchunguzi wa afya.
アンナ 何時からですか。 Kuanzia saa ngapi?
Anna NANJI KARA DESU KA.
Kuanzia saa ngapi?
先生 午前9時から11時までです。
ここに8時半に集まって下さい。
Kuanzia saa tatu hadi saa tano asubuhi.
Tafadhali tukusanyike hapa saa mbili na nusu.
Mwalimu GOZEN KUJI KARA JÛICHIJI MADE DESU. KOKO NI HACHIJI HAN NI ATSUMATTE KUDASAI.
Kuanzia saa tatu hadi saa tano asubuhi.
Tafadhali tukusanyike hapa saa mbili na nusu.

Vidokezo vya sarufi

NANJI

NAN inamaanisha "nini" na JI ni kiambishi cha kutaja saa kamili.
k.m.) NANJI DESU KA. (Ni saa ngapi?)
Tafadhali angalia "Nyenzo za kujifunzia."

Mwalimu Tufundishe

Vitenzi vya umbo la TE - Namna mbalimbali
Katika somo lililotangulia ulijifunza namna rahisi ya kubadilisha kitenzi cha umbo la MASU iwe kitenzi cha umbo la TE. Unachofanya ni kubadilisha MASU iwe TE.

Tanakali Sauti

Nusura ifike kikomo
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Nilisikia kuna namba ambazo zinachukuliwa kama bahati mbaya nchini Japani. Nne ambayo hutamkwa SHI, matamshi yake pia humaanisha “kifo”. Tisa ambayo hutamkwa KU, matamshi yake pia humaanisha “matatizo.” Kwa hiyo baadhi ya hoteli au hospitali zinakwepa kuweka namba 4 na 9 kwenye vumba vyao.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.