NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 6

Somo la 6

Namba yako ya simu ni ipi?

Anna na Sakura wanaendelea na mazungumzo yao chumbani mwa Anna. Sakura anamwuliza Anna namba yake ya simu.

Somo la 6 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

DENWABANGÔ WA NANBAN DESU KA

Mazungumzo

さくら ところでアンナさん。
電話番号は何番ですか。
Anna, licha ya hivyo, namba yako ya simu ni ipi?
Sakura TOKORODE ANNA-SAN. DENWABANGÔ WA NANBAN DESU KA.
Anna, licha ya hivyo, namba yako ya simu ni ipi?
アンナ ええと。080-1234-・・・。 Ee.... 080 – 1234 – ....
Anna ÊTO. REI HACHI REI - ICHI NI SAN YON - ...
Ee.... 080 – 1234 – ....
さくら ありがとう。
じゃ、今度、電話をしますね。
Asante. Basi, nitakupigia wakati mwingine.
Sakura ARIGATÔ. JA, KONDO, DENWA O SHIMASU NE.
Asante. Basi, nitakupigia wakati mwingine.

Vidokezo vya sarufi

Namba (1)

Tujifunze kuanzia sifuri hadi kumi.
Tafadhali nenda kwenye "Nyenzo za kujifunzia."

  O SHIMASU

SHIMASU ni ktenzi kinachomaanisha "kufanya kitu fulani."
Unaweza kuzungumzia vitendo vingi kwa kuijumuisha na nomino.
k.m.)
BENKYÔ (kusoma) + O SHIMASU
= BENKYÔ O SHIMASU (Ninasoma)  
RYÔRI (kupika) + O SHIMASU
= RYÔRI O SHIMASU (Ninapika)

Mwalimu Tufundishe

Herufi HA inapotamkwa kama WA
Katika siku za nyuma, WA inayoonyesha mada ilitamkwa na kuandikwa kama HA. Matamshi yake yamebadilika polepole na kuwa WA, lakini bado inaandikwa kama HA. Utaratibu huo unaweza kuwa vivyo hivyo kwa WA kwenye neno la KONNICHIWA (habari za mchana?). Inatamkwa kama WA, lakini inaandikwa kama HA.

Tanakali Sauti

Simu
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Nikipokea simu, ninachotakiwa kusema ni MOSHI MOSHI, kisha niseme jina langu. Nataka kusema ‘HAI, MOSHI MOSHI, ANNA DESU.’ Ninatamani mtu yeyote anipigie simu haraka iwezekanavyo.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.