NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 48

Somo la 48

Asante kwa yote

Leo, Anna anarejea nchini Thailand. Sakura na Kenta wamekwenda uwanja wa ndege kumuaga.

Somo la 48 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

IROIRO OSEWA NI NARIMASHITA

Mazungumzo

健太 体に気をつけて。 Nakutakia afya njema.
Kenta KARADA NI KIOTSUKETE.
Nakutakia afya njema.
さくら タイに着いたら連絡してね。 Ukiwasili nchini Thailand, tafadhali tujulishe.
Sakura TAI NI TSUITARA, RENRAKU SHITE NE.
Ukiwasili nchini Thailand, tafadhali tujulishe.
アンナ はい。いろいろお世話になりました。 Sawa. Asante kwa yote.
Anna HAI. IROIRO OSEWA NI NARIMASHITA.
Sawa. Asante kwa yote.
アンナ 健太さんとさくらさんもお元気で。 Kenta na Sakura, pia nawatakia afya njema.
Anna KENTA-SAN TO SAKURA-SAN MO OGENKIDE.
Kenta na Sakura, pia nawatakia afya njema.

Vidokezo vya sarufi

KIOTSUKETE

KIOTSUKETE ni umbo la TE la kitenzi KIOTSUKEMASU (kuwa mwangalifu). Unatumia NI kuonyesha kile unachotakiwa kuwa makini nacho.
k.m.) KURUMA NI KIOTSUKETE.
(Kuwa mwangalifu na magari.)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kuboresha Kijapani chako
Umekuwa ukijifunza mambo ya msingi katika lugha ya Kijapani kwa mwaka mmoja.

Tanakali Sauti

Kicheko
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Kila mmoja, SAYÔNARA (kwa heri), hadi tutakapokutana tena. Nitakapokuja Japani wakati mwingine, nitakuwa ninazungumza Kijapani kwa ufasaha zaidi. U FU FU!

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.