NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 46

Somo la 46

Nimefurahi kuona theluji, kabla ya kurejea nchini kwangu

Baada ya kusherehekea kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya Anna, Kenta alijitolea kumrejesha bwenini. Walipotoka, theluji ikaanza kudondoka.

Somo la 46 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

KIKOKU SURU MAE NI, YUKI O MIRU KOTO GA DEKITE SHIAWASE DESU

Mazungumzo

アンナ もしかして、雪? Hii ni theluji, au?
Anna MOSHIKASHITE, YUKI?
Hii ni theluji, au?
健太 これは、粉雪。
粉のようにさらさらしているでしょ。
Hii ni theluji ya ungaunga.
Ni nyepesi, kavu na laini kama unga, au siyo?
Kenta KORE WA, KONAYUKI.
KONA NO YÔ NI SARASARA SHITEIRU DESHO.
Hii ni theluji ya ungaunga. Ni nyepesi, kavu na laini kama unga, au siyo?
アンナ 帰国する前に、雪を見ることができて幸せです。 Nimefurahi kuona theluji, kabla ya kurejea nchini kwangu.
Anna KIKOKU SURU MAE NI, YUKI O MIRU KOTO GA DEKITE SHIAWASE DESU.
Nimefurahi kuona theluji, kabla ya kurejea nchini kwangu.

Vidokezo vya sarufi

  NO YÔ NI

NO YÔ NI inamaanisha "kama _".
k.m.) KONA NO YÔ NI (kama ungaunga)

Mwalimu Tufundishe

Umbo la kikamusi + MAE NI
MAE NI (kabla ya) ni kauli ya kusisitiza unachofanya au ulichofanya, kabla ya kufanya kitu kingine. Vitenzi huwa kwenye umbo la kikamusi, ikiwa vitafuatiwa na MAE NI. Hata kama sentensi yote iko katika hali ya wakati uliopita, kitenzi kinachukua umbo la kikamusi kabla ya MAE NI, japo umbo hili linaashiria wakati uliopo.

Tanakali Sauti

Theluji
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Theluji nyepesi inaitwa KONAYUKI. Theluji iliyo majimaji ni BOTANYUKI. Watu husema vipande vikubwa vya theluji vinaonekana kama petali za maua ya BOTAN.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.