NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 44

Somo la 44

Baada ya kula vitamutamu vya Kijapani, unakunywa chai ya kijani.

Baada ya kutembelea kasri la Himeji, Anna amehudhuria hafla ya chai kwenye nyumba iliyo karibu ambapo hafla hiyo hufanyika.

Somo la 44 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

WAGASHI O TABETE KARA, MACCHA O NOMIMASU.

Mazungumzo

アンナ 和菓子はとても甘いですね。 Vitamutamu vya Kijapani ni vitamu sana, au siyo?
Anna WAGASHI WA TOTEMO AMAI DESU NE.
Vitamutamu vya Kijapani ni vitamu sana, au siyo?
先生 和菓子を食べてから、抹茶を飲みます。
抹茶は苦いかもしれません。
Baada ya kula vitamutamu vya Kijapani, unakunywa chai ya kijani.
Chai hiyo inaweza kuwa chungu.
Mwalimu WAGASHI O TABETE KARA, MACCHA O NOMIMASU.
MACCHA WA NIGAI KAMOSHIREMASEN.
Baada ya kula vitamutamu vya Kijapani, unakunywa chai ya kijani. Chai hiyo inaweza kuwa chungu.
アンナ 先生、足がしびれました。いたたたた。 Mwalimu, miguu yangu imekufa ganzi. Ah, ah, ah, uui!
Anna SENSEI, ASHI GA SHIBIREMASHITA. ITATATATA.
Mwalimu, miguu yangu imekufa ganzi. Ah, ah, ah, uui!

Vidokezo vya sarufi

  KAMOSHIREMASEN

KAMOSHIREMASEN inaamisha "inaweza kuwa."
k.m.) NIGAI KAMOSHIREMASEN. (Inaweza kuwa chungu.)

Mwalimu Tufundishe

Umbo la TE la kitenzi + KARA
Katika somo la 16, ulijifunza kwamba unaweza kuelezea zaidi ya tukio moja kwenye sentensi moja kwa kuunganisha vitenzi vya umbo la TE.

Tanakali Sauti

Kufa ganzi
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Kuketi huku umekunja miguu yako ni jambo gumu. Nimeelekezwa namna nzuri ya kuzuia miguu isife ganzi. Ni kuketi huku vidole gumba vya miguuni vikiwa pamoja. Wakati mwingine nitajaribu kuketi hivyo.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.