NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 40

Somo la 40

Kichwa kinauma.

Anna amepata homa na amelala chumbani mwake. Mama msimamizi wa bweni ana wasiwasi na amekwenda kumuangalia anavyoendelea.

Somo la 40 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

ATAMA GA ZUKIZUKI SHIMASU

Mazungumzo

寮母 おかゆですよ。
体調は、どう?
Huu ni uji wa mchele.
Unajisikiaje?
Msimamizi wa bweni OKAYU DESU YO.
TAICHÔ WA, DÔ?
Huu ni uji wa mchele. Unajisikiaje?
アンナ 頭がずきずきします。 Kichwa kinauma.
Anna ATAMA GA ZUKIZUKI SHIMASU.
Kichwa kinauma.
寮母 そう。欲しいものがあったら、言ってね。 Kumbe. Ikiwa kuna kitu unataka, niambie.
Msimamizi wa bweni SÔ. HOSHII MONO GA ATTARA, ITTE NE.
Kumbe. Ikiwa kuna kitu unataka, niambie.

Vidokezo vya sarufi

Tanakali sauti + SHIMASU

ZUKIZUKI ni tanakali sauti. Unaweza kuitumia unapoumwa na kichwa, na kuhisi kinagonga. Ikiwa itaunganishwa na SHIMASU (kufanya), neno hilo linakuwa kitenzi.
k.m.) ZUKIZUKI SHIIMASU (kuuma)

Mwalimu Tufundishe

Makundi matatu ya vitenzi
Vitenzi vya Kijapani vimegawanyika katika makundi matatu. Kila kundi lina namna yake ya mnyambuliko.

Tanakali Sauti

kuhisi kuugua
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Nchini Japani ikiwa huna hamu ya kula, chakula mbadala ni uji wa mchele. Pia tufaha zilizoparuzwa ni maarufu. Vyote ni vyakula vyepesi na rahisi kusagika tumboni.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.