NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 4

Somo la 4

Nimerudi hivi sasa.

Anna amerudi bwenini na Sakura. Msimamizi wa bweni amekuja mlangoni kuwasalimia.

Somo la 4 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

TADAIMA

Mazungumzo

アンナ ただいま。 Nimerudi hivi sasa.
Anna TADAIMA.
Nimerudi hivi sasa.
寮母 お帰りなさい。 Karibu.
Dorm Mother OKAERINASAI.
Karibu.
さくら こんにちは。 Habari za mchana?
Sakura KONNICHIWA.
Habari za mchana?
寮母 あなたも留学生ですか。 Wewe pia ni mwanafunzi wa kigeni?
Dorm Mother ANATA MO RYÛGAKUSEI DESU KA.
Wewe pia ni mwanafunzi wa kigeni?
さくら いいえ、私は留学生ではありません。
日本人の学生です。
Hapana, mimi si mwanafunzi wa kigeni.
Mimi ni mwanafunzi Mjapani.
Sakura IIE, WATASHI WA RYÛGAKUSEI DEWA ARIMASEN.
NIHON-JIN NO GAKUSEI DESU.
Hapana, mimi si mwanafunzi wa kigeni. Mimi ni mwanafunzi Mjapani.

Vidokezo vya sarufi

  DEWA ARIMASEN

DESU ni neno la kiungwana linalomalizia sentensi.
k.m.) HAI, WATASHI WA NIHON-JIN DESU. (Ndiyo, mimi ni Mjapani.)

DEWA ARIMASEN ni umbo la kukanusha la DESU.
k.m.) IIE, WATASHI WA NIHON-JIN DEWA ARIMASEN. (Hapana, mimi siyo Mjapani.)
Kwa kujifunza zaidi, tafadhali usome "Mwalimu, tufundishe."

Mwalimu Tufundishe

Jinsi ya kutengeneza sentensi za kukanusha
Tuchukulie mfano huu, "Mimi ni Mjapani."

Tanakali Sauti

Milango
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Sakura alipoingia bwenini alivua viatu vyake, na kuvigeuza halafu akaviweka vizuri kwenye sehemu ya kuingilia. Pia mimi nitafanya vivyo hivyo nitakapomtembelea mtu yeyote nyumbani kwake!

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.