NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 39

Somo la 39

Nafikiri una homa.

Anna hahisi vizuri, na amekwenda hospitalini, akiwa ameambatana na mama msimamizi wa bweni. Sasa anamwona daktari.

Somo la 39 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

KAZE DA TO OMOIMASU

Mazungumzo

医者 どうしましたか。 Una tatizo gani?
Daktari DÔ SHIMASHITA KA.
Una tatizo gani?
アンナ せきが出ます。 Nina kikohozi.
Anna SEKI GA DEMASU.
Nina kikohozi.
寮母 熱も37.8度あります。 Pia ana joto la mwili nyuzi 37.8.
Msimamizi wa bweni NETSU MO SANJÛNANA TEN HACHI DO ARIMASU.
Pia ana joto la mwili nyuzi 37.8.
医者 喉を見せてください。
かぜだと思います。
Tafadhali nionyeshe koo lako.
Nafikiri una homa.
Daktari NODO O MISETE KUDASAI.
KAZE DA TO OMOIMASU.
Tafadhali nionyeshe koo lako. Nafikiri una homa.

Vidokezo vya sarufi

Dalili

Elezea dalili zako.
ATAMA GA ITAI DESU. (Kichwa kinauma.)
HANAMIZU GA DEMASU. (Nina mafua.)
ONAKA GA ITAI DESU. (Tumbo linauma.)

Mwalimu Tufundishe

Nafikiri kwamba
Unapoelezea fikra, maoni au makisio yako, kwanza unasema kile unachofikiria, na kisha unasema TO OMOIMASU, (Nafikiri kwamba). OMOIMASU ni kitenzi kinachomaanisha (kufikiri). Unaongeza TO baada ya kile unachofikiria.

Tanakali Sauti

kukohoa
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Keshia aliye hospitalini na pia mfamasia waliniambia,
“ODAIJINI” yaani (ugua pole). Kila mmoja alikuwa na wasiwasi kunihusu, na hilo lilinifanya nikaanza kuhisi wananijali. Natumai nitapona haraka iwezekanavyo.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.