NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 38

Somo la 38

Sawa.

Anna alipoamka asubuhi, alihisi uchovu na homa. Anakwenda hospitalini pamoja na Mama msimamizi wa bweni.

Somo la 38 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

KASHIKOMARIMASHITA

Mazungumzo

寮母 市民病院までお願いします。 Tafadhali tupeleke hospitali ya umma.
Msimamizi wa bweni SHIMIN BYÔIN MADE ONEGAI SHIMASU.
Tafadhali tupeleke hospitali ya umma.
運転手 かしこまりました。 Sawa mama.
Dereva wa teksi KASHIKOMARIMASHITA.
Sawa mama.
寮母 まっすぐ行って、3つ目の信号を左に曲がってください。 Tafadhali nenda moja kwa moja, kisha pinda kushoto kwenye taa ya tatu.
Msimamizi wa bweni MASSUGU ITTE, MITTSU ME NO SHINGÔ O HIDARI NI MAGATTE KUDASAI.
Tafadhali nenda moja kwa moja, kisha pinda kushoto kwenye taa ya tatu.

Vidokezo vya sarufi

Kauli ya heshima

Unatumia kauli ya heshima unapozungumza na, au unapomtaja mtu aliyekuzidi umri, kiongozi wako, mwalimu, wateja, au mtu ambaye humfahamu vizuri.
Ili kujifunza zaidi, tafadhali nenda "Mwalimu Tufundishe."


Mwalimu Tufundishe

Kauli ya heshima
Unatumia kauli ya heshima unapozungumza na, au unapomtaja mtu aliyekuzidi umri, kiongozi wako, mwalimu, wateja, au mtu ambaye humfahamu vizuri.

Tanakali Sauti

Kushindwa kusimama / kuhisi kizunguzungu
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Madereva wa teksi nchini Japani huwafungulia wateja milango. Ikiwa utajaribu kujifungulia mlango mwenyewe, utakatazwa. Kwa hiyo kuwa muangalifu.”

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.