NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 37

Somo la 37

Niliona mlima Fuji, nikala sushi na kadhalika.

Anna amerejea bwenini jijini Tokyo kutoka mji wa Shizuoka. Anamueleza mama msimamizi wa bweni jinsi safari yake ilivyokuwa.

Somo la 37 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

FUJISAN O MITARI, OSUSHI O TABETARI SHIMASHITA

Mazungumzo

寮母 旅行はどうだった? Safari yako ilikuwaje?
Msimamizi wa bweni RYOKÔ WA DÔ DATTA?
Safari yako ilikuwaje?
アンナ 富士山を見たり、おすしを食べたりしました。楽しかったです。 Niliona mlima Fuji, nikala sushi, na kadhalika. Nilifurahia.
Anna FUJISAN O MITARI, OSUSHI O TABETARI SHIMASHITA.
TANOSHIKATTA DESU.
Niliona mlima Fuji, nikala sushi, na kadhalika. Nilifurahia.
寮母 それはよかったわね。 Ilikuwa nzuri.
Msimamizi wa bweni SORE WA YOKATTA WA NE.
Ilikuwa nzuri.

Vidokezo vya sarufi

  WA DÔ DATTA?

DÔ inaamisha "vipi/namna gani." DATTA ni umbo la kawaida la DESHITA, ambalo humalizia sentensi kwa hali ya wakati uliopita.                                                                          k.m.) SHIKEN WA DÔ DATTA? (Mtihani ulikuwaje?)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kuonyesha mifano kwa kutumia TARI
Unapotoa mifano miwili ama mitatu miongoni mwa vitendo kadhaa, unatumia vitenzi vya umbo la TA na kuongeza RI baada ya kila kitenzi cha umbo la TA kwa mfuatano. Mwishoni, unamalizia sentensi kwa kutumia SHIMASU (nafanya), SHIMASHITA (nilifanya), au SHITAI DESU (ninataka kufanya).

Tanakali Sauti

Uchovu
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Zawadi niliyomletea mama msimamizi wa bweni kutoka Shizuoka ni biskuti zilizo na ladha ya chai ya Kijani. Ilikuwa vigumu kuchagua cha kumletea. Kulikuwa na peremende na chokleti zilizo na ladha ya chai na vingine vingi.
Wajapani ni hodari katika kubuni bidhaa mpya!

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.