Somo la 33
Anna, nitakupatia.

Anna amekwenda kwenye tamasha la chuo kikuu pamoja na Kenta ambaye ni binamu yake Sakura. Wanaangalia maonyesho ya picha yaliyoandaliwa na klabu ya upigaji picha.
Usemi wa msingi:
ANNA-SAN NI AGEMASU
Mazungumzo
健太 | これは、僕が富士山で撮った写真です。 | Hii ni picha niliyopiga nikiwa mlima Fuji.
|
---|---|---|
Kenta | KORE WA, BOKU GA FUJISAN DE TOTTA SHASHIN DESU.
Hii ni picha niliyopiga nikiwa mlima Fuji.
|
|
アンナ | あっ、私だ。 | Oh, yule ni mimi.
|
Anna | A', WATASHI DA.
Oh, yule ni mimi.
|
|
健太 | 驚いた? あとで、アンナさんにあげます。 |
Umeshangaa? Anna, nitakupatia baadaye. |
Kenta | ODOROITA? ATODE, ANNA-SAN NI AGEMASU. Umeshangaa? Anna, nitakupatia baadaye.
|
|
アンナ | 写真をくれるんですか。うれしいです。 | Utanipatia picha? Nitafurahi.
|
Anna | SHASHIN O KURERU N DESU KA? URESHII DESU.
Utanipatia picha? Nitafurahi.
|
Vidokezo vya sarufi
AGEMASU na KUREMASU
Katika Kijapani vitenzi tofauti hutumika, kutegemea mtazamo wa mtoaji au mpokeaji.
Wakati mzungumzaji anapompatia kitu msikilizaji, anasema AGEMASU. Ikiwa mtu fulani atakupatia kitu, tumia neno KUREMASU.
Kwa kujifunza zaidi, tafadhali usome kona ya "Mwalimu, tufundishe."
Mwalimu Tufundishe
Tofauti kati ya AGEMASU na KUREMASU
katika Kijapani vitenzi tofauti hutumika, kutegemea mtazamo wa mtoaji au mpokeaji.
Tanakali Sauti
Tabasamu
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Kwenye tamasha la chuoni, kulikuwa na vibanda vya vyakula. Nilikula tambi za kukaangwa, yakisoba. Inasemekana msimu wa pukutizi ni msimu wa sanaa, michezo na vilevile hamu ya kula. Kwa kweli huu ni msimu mzuri!
