Somo la 3
Msalani ni wapi?
Leo, Sakura anamtembeza Anna Chuoni.
Usemi wa msingi:
TOIRE WA DOKO DESU KA
Mazungumzo
さくら | ここは教室です。 | Hili ni darasa.
|
---|---|---|
Sakura | KOKO WA KYÔSHITSU DESU.
Hili ni darasa.
|
|
アンナ | わあ、広い。 | Oh, ni pana.
|
Anna | WÂ, HIROI.
Oh, ni pana.
|
|
さくら | あそこは図書館。 | Pale ni maktaba.
|
Sakura | ASOKO WA TOSHOKAN.
Pale ni maktaba.
|
|
アンナ | トイレはどこですか。 | Msalani ni wapi?
|
Anna | TOIRE WA DOKO DESU KA.
Msalani ni wapi?
|
|
さくら | すぐそこです。 | Ni hapo tu.
|
Sakura | SUGU SOKO DESU.
Ni hapo tu.
|
Vidokezo vya sarufi
WA DOKO DESU KA
(_ ni wapi?)
DOKO DESU KA ni kifungu cha maneno kinachotumika wakati wa kuuliza mahali.
k.m.) TOIRE WA DOKO DESU KA. (Msalani ni wapi?)
Mwalimu Tufundishe
Vionyeshi
Vionyeshi ni maneno tunayoyatumia iwapo tunaonyesha vitu, watu au mahali. Vinaitwa maneno ya KO-SO-A-DO, ambayo yanachukua silabi ya kwanza ya vionyeshi vya makundi manne.
Tanakali Sauti
Wanyama wanaotembea
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Nilipouliza "TOIRE WA DOKO DESU KA," watu walinifahamisha. Nilieleweka nilipozungumza Kijapani. Sasa ninaweza kutafuta njia ya kwenda popote ninapotaka.