NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 27

Somo la 27

Nani anayeolewa?

Anna amemtembelea rafiki yake Sakura nyumbani mwake. Sakura alimuonyesha Anna kadi ya mwaliko wa harusi.

Somo la 27 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

DARE GA KEKKON SURU N DESU KA

Mazungumzo

アンナ 誰が結婚するんですか。 Nani anayeolewa?
Anna DARE GA KEKKON SURU N DESU KA.
Nani anayeolewa?
さくら 静岡の友だち。 Rafiki wa mkoani Shizuoka.
Sakura SHIZUOKA NO TOMODACHI.
Rafiki wa mkoani Shizuoka.
アンナ へえ。いつですか。 Kumbe. Ni lini?
Anna HÊ. ITSU DESU KA.
Kumbe. Ni lini?
さくら 来月20日よ。アンナも一緒に静岡に行かない? Tarehe 20 mwezi ujao. Anna, kwa nini tusiende pamoja Shizuoka?
Sakura RAIGETSU HATSUKA YO. ANNA MO ISSHO NI SHIZUOKA NI IKANAI?
Tarehe 20 mwezi ujao. Anna, kwa nini tusiende pamoja Shizuoka?

Vidokezo vya sarufi

Umbo la NAI la kitenzi + ?

Unapotamka umbo la NAI la kitenzi kwa toni ya juu, unamtaka mtu kufanya jambo fulani kwa njia ya kawaida.

k.m.)  ISSHO NI EIGA O MINAI?
(Kwa nini tusiangalie filamu pamoja?)

Kwa njia ya kiungwana, unasema hivi:
ISSHO NI EIGA O MIMASENKA?
(Unaonaje tukiangalia filamu pamoja?)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kutamka tarehe
Kwa Kijapani, tarehe mosi ni TSUITACHI.

Tanakali Sauti

Milio ya wanyama
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Nitakwenda na Sakura katika mji wake wa nyumbani wa Shizuoka. Nilifikiria ningehudhuria sherehe ya harusi na Sakura. Lakini haiwezekani. Huwezi kuhudhuria bila kadi ya mwaliko.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.