NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 26

Somo la 26

Tujitahidi wakati mwingine.

Leo, Anna amepata matokeo ya mtihani wa Kijapani. Alimuona mwanafunzi mwenzake Rodrigo akiwa ameinamisha kichwa chake.

Somo la 26 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

TSUGI WA GANBARÔ

Mazungumzo

アンナ ロドリゴ、元気がないね。 Rodrigo, unaonekana hauko sawa.
Anna RODORIGO, GENKI GA NAI NE.
Rodrigo, unaonekana hauko sawa.
ロドリゴ 試験ができなかったんです。 Sikufanya vizuri katika jaribio.
Rodrigo SHIKEN GA DEKINAKATTA N DESU.
Sikufanya vizuri katika jaribio.
アンナ 私も…。60点でした。
次はがんばろう。
Mimi pia.... Nimepata alama 60.
Tujitahidi wakati mwingine.
Anna WATASHI MO.... ROKUJITTEN DESHITA.
TSUGI WA GANBARÔ.
Mimi pia.... Nimepata alama 60. Tujitahidi wakati mwingine.

Vidokezo vya sarufi

  N DESU

Unasema N DESU, unapoelezea hali au sababu. Kabla ya N DESU, unatakiwa kutumia muundo wa kawaida wa kitenzi, kama vile umbo la kikamusi na umbo la TA.
k.m.) SHIKEN GA DEKINAKATTA N DESU. 
(Sikufanya vizuri katika jaribio.)

DESHITA

DESHITA ni umbo la wakati uliopita la DESU.
k.m.) TAIHEN DESU. (Ni vigumu.)
>> TAIHEN DESHITA. (Ilikuwa vigumu.)

Mwalimu Tufundishe

Umbo la kuonyesha nia la vitenzi
GANBARÔ, (Tujitahidi), ni aina ya mnyambuliko wa vitenzi unaofahamika kama “umbo la kuonyesha nia.” Inaelezea dhamira ya mzungumzaji. Pia hutumika kumshirikisha msikilizaji kufanya jambo fulani pamoja au kumtaka afanye jambo fulani. Huwezi kutumia usemi huu kwa wakuu wako.

Tanakali Sauti

Kulia
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Rodrigo alipata alama 80 kwenye jaribio. Alifanya vizuri kunishinda. Sikuwa na haja ya kuwa na wasiwasi juu yake.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.