NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 23

Somo la 23

Nilikaripiwa na mama msimamizi wa bweni.

Anna alipokuwa akiongea na Sakura chuoni, aliulizwa kuhusiana na siku aliporudi bwenini kwa kuchelewa.

Somo la 23 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

OKÂSAN NI SHIKARAREMASHITA

Mazungumzo

さくら この間は門限に間に合った? Siku ile ulifika bwenini kwa wakati?
Sakura KONOAIDA WA MONGEN NI MANIATTA?
Siku ile ulifika bwenini kwa wakati?
アンナ いいえ。間に合いませんでした。
それで、お母さんに叱られました。
Hapana. Sikuwahi.
Kwa hiyo, nilikaripiwa na mama msimamizi wa bweni.
Anna IIE. MANIAIMASEN DESHITA.
SOREDE, OKÂSAN NI SHIKARAREMASHITA.
Hapana. Sikuwahi. Kwa hiyo, nilikaripiwa na mama msimamizi wa bweni.
アンナ 掃除当番が3回増えました。 Jukumu langu la kufanya usafi limeongezeka mara tatu zaidi.
Anna SÔJI TÔBAN GA SANKAI FUEMASHITA.
Jukumu langu la kufanya usafi limeongezeka mara tatu zaidi.
さくら それは大変だったね。 Ilikuwa vigumu, au siyo?
Sakura SORE WA TAIHEN DATTA NE.
Ilikuwa vigumu, au siyo?

Vidokezo vya sarufi

  MASEN DESHITA

Badilisha vitenzi vya umbo la MASU katika hali ya kukanusha inayoashiria wakati uliopita kwa kubadilisha MASU kuwa MASEN DESHITA.

k.m.)
MANIAIMASU (kuwahi)  
>> umbo la kukanusha: MANIAIMASEN (kutowahi)
>> umbo la kukanusha ya wakati uliopita: MANIAIMASEN DESHITA (sikuwahi)

Mwalimu Tufundishe

Kauli ya kutendewa
Unatumia umbo la kutendewa, ikiwa unazungumza kwa mtazamo wa mtu aliyetendewa jambo. Ili kufanya hivyo, unatumia kitenzi cha umbo la kutendewa na uelezee ni nani aliyetenda kitendo hicho kwa kutumia NI. 

Tanakali Sauti

Kufanya usafi
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Kufanya usafi kunachosha. Lakini ukimaliza, kila kitu huonekana PIKA PIKA (hung’aa). Inafurahisha.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.