NHK WORLD > Jifunze Kijapani > Mwanzo wa ukurasa wa Kiswahili > Orodha ya Masomo > Somo la 22

Somo la 22

Nimechelewa.

Anna alifurahia katika kibanda cha Karaoke na rafiki zake kiasi kwamba alirejea bwenini akiwa amechelewa.

Somo la 22 (Dakika 10)

Usemi wa msingi:

OSOKU NARIMASHITA

Mazungumzo

アンナ お母さん、ごめんなさい。遅くなりました。 Mama, samahani. Nimechelewa.
Anna OKÂSAN, GOMENNASAI. OSOKU NARIMASHITA.
Mama, samahani. Nimechelewa.
寮母 アンナさん、10分も遅刻です。
約束を破ってはいけません。
Anna, umechelewa kwa dakika 10.
Usivunje ahadi.
Msimamizi wa bweni ANNA-SAN, JIPPUN MO CHIKOKU DESU.
YAKUSOKU O YABUTTE WA IKEMASEN.
Anna, umechelewa kwa dakika 10. Usivunje ahadi.
アンナ すみません。気をつけます。 Samahani. Nitakuwa mwangalifu.
Anna SUMIMASEN. KI O TSUKEMASU.
Samahani. Nitakuwa mwangalifu.

Vidokezo vya sarufi

FUN / PUN: kiambishi cha kutaja dakika

dakika 2 = NIFUN
dakika 10 = JIPPUN / JUPPUN

Ukitaka kujifunza namna ya kutaja dakika 1 hadi 10, nenda ukurasa wa "Nyenzo za kujifunzia."

Umbo la TE la kitenzi + WA IKEMASEN

Ukitumia kitenzi cha umbo la TE na kuongeza WA IKEMASEN, utamaanisha "Usifanye hivyo."
k.m.)
YAKUSOKU O YABUTTE WA IKEMASEN.
(Usivunje ahadi.)

Mwalimu Tufundishe

Namna ya kubadilisha vivumishi kuwa vielezi
Vivumishi vya Kijapani vinanyambulika na kuwa vielezi.

Tanakali Sauti

Hasira
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.

Tafakuri ya Anna

Nimemtia wasiwasi sana mama msimazi wa bweni. Nimejifunza ya kwamba ikiwa nitachelewa, Ninastahili kutoa taarifa mapema.

Anna

Orodha ya Masomo

*Utatoka kwenye tovuti ya NHK.