Somo la 18
Nimepotea njia.

Anna alitembelea duka la kuuza vitabu pamoja na rafiki zake, Sakura na Rodrigo. Baada ya kuondoka kwenye duka hilo, Anna alipoteleana na wenzake.
Usemi wa msingi:
MICHI NI MAYOTTE SHIMAIMASHITA
Mazungumzo
アンナ | もしもし、さくらさん。助けてください。 道に迷ってしまいました。 |
Halo, Sakura. Tafadhali nisaidie.
Nimepotea njia.
|
---|---|---|
Anna | MOSHIMOSHI, SAKURA-SAN. TASUKETE KUDASAI. MICHI NI MAYOTTE SHIMAIMASHITA. Halo, Sakura. Tafadhali nisaidie.
Nimepotea njia.
|
|
さくら | 今、どこ? | Uko wapi hivi sasa?
|
Sakura | IMA, DOKO?
Uko wapi hivi sasa?
|
|
アンナ | 目の前に郵便局があります。 | Mbele yangu kuna ofisi ya posta.
|
Anna | ME NO MAE NI YÛBINKYOKU GA ARIMASU.
Mbele yangu kuna ofisi ya posta.
|
|
さくら | 分かった。そこにいて。 | Nimeelewa. Baki hapo ulipo.
|
Sakura | WAKATTA. SOKO NI ITE.
Nimeelewa. Baki hapo ulipo.
|
Vidokezo vya sarufi
Kitenzi cha umbo la TE + SHIMAIMASHITA
Unasema SHIMAIMASHITA baada ya kitenzi cha umbo la TE ili kuonyesha umefanya jambo bila uangalifu au unajutia ulichokifanya.
k.m.)
MACHIGAEMASU (kukosea)
>> MACHIGAETE SHIMAIMASHITA (Nimekosea)
Ili kujifunza zaidi, tafadhali soma "Mwalimu, Tufundishe."
Mwalimu Tufundishe
Kitenzi cha umbo la TE + SHIMAIMASHITA
Ukisema SHIMAIMASHITA baada ya kitenzi cha umbo la TE, unasema ya kwamba umemaliza au umekamilisha jambo ulilokuwa ukifanya, na huwezi kulirejesha katika hali yake ya awali. Kwa hiyo mara nyingi unatumia SHIMAIMASHITA, ikiwa umekosea kufanya jambo fulani na unajutia.
Tanakali Sauti
Kuchanganyikiwa / kuzunguka bila kujua cha kufanya
Kijapani ni lugha iliyo na tanakali sauti nyingi. Kwenye lugha ya Kijapani kuna aina nyingi za tanakali sauti, kuanzia sauti zinazotolewa na wanyama hadi namna ya kuelezea hisia. Yote hayo yameelezwa kwa sauti. Tafadhali bofya kitufe cha kusikiliza na ufurahie.
Tafakuri ya Anna
Niliambiwa ikiwa nimepotea njia, ninaweza kwenda kwenye kituo cha polisi. Afisa wa polisi ataniambia muelekeo kwa kunionyesha ramani.
